Google PlusRSS FeedEmail

MUZIKI WA BONGO UNAIGWA ULAYA

Nyota wa muziki wa kizazi kipya ambaye pia ni muandaaji wa muziki Dully Sykes, amesema kuwa hata wasanii wa nje wamekuwa wakiiga baadhi ya vionjo kutoka Afrika lakini inashangaza kuona kwamba hakuna mtu yoyote anayezungumzia ukweli huo.Msanii huyo aliyekuwa akizungumza katika kipindi cha Powerjams kinachorushwa na kituo cha East Africa,alisema kinyume chake msanii wa nyumbani akifanya jambo kama hilo huwa ni tatizo linaonekana  Aliongeza kwamba ‘sample’kwenye muziki wa hip pop ni kitu cha kawaida.Dully alitoa ufafanuzi huo wakati alipohojiwa katika kipindi cha Powerjams kuhusu wimbo alioutengeneza yeye na kuonekana ukifanana na wimbo wa ‘Hey’ wa msanii Cecile kutoka Jamaica Dully alisema kuwa watu wanatakiwa waelewe kuwa ‘sample’kwenye muziki wa hip pop ni kitu cha kawaida na kwamba vilevile aina ya wimbo ambao wao wameuiga ni staili ya riddim ambayo kwa kawaida si kosa kwa msanii kutumia mapigo hayo kuandaa wimbo wake "Ni kitu ambacho kinafanyika na waandaaji wa muziki kama wakina Timbaland wanafanya hivi vitu na muziki wao unafanya vizuri duniani mpaka huku sisi tunaupenda kwanini mimi ambaye bado sijafikia mafanikio yao nisifanye hivyo ili nifanye vizuri ni vitu vingi tunaiga kutoka nchi za wenzetu " alisema Dully  Msanii huyo alisema kuwa mashabiki wa muziki wa kizazi kipya bado hawaamini kuwa hata hao wasanii wa nje kuna nyimbo ambazo wanaiga kutoka huku Afrika

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging