Google PlusRSS FeedEmail

NEY WA MITEGO AWASHUKIA BONGO MOVIE.

Msanii wa muziki wa kizazi kipya Bongo fleva Emmanuel Elbariki ‘Ney wa Mitego’ amewashukia wasanii wanaounda kundi la Bongo Movie Stars  kwa kusema kuwa wameshindwa kutengeneza filamu zenye ujumbe na badala yake wanatumia filamu hizo kwa ajili ya kuuza sura tu na akina dada kupata njia ya kujiuza kupitia filamu hizo, lakini hakuna filamu zenye viwango vya kuridhisha.“Bongo movie hakuna kitu zaidi ya biashara zao za ukahaba tu, ndio maana mara nyingi utaona akina dada wakivaa vimini na nguo zinazoweza kuonyesha mapaja kwa ajili ya kuwachanganya wapenda wanawake, kuna watu wanaweza kuwatetea mimi nina ushahidi kuna rafiki zangu wengi wamefanya nao biashara ya mapenzi, kwa sababu ni washikaji zangu siwezi kuwataja, mara nyingi nikiimba najua ukweli, kama wanaigiza waigize na kuachana na biashara nyingine,”anasema Ney wa Mitego.Ney kutokana na kutokuridhishwa ameamua kuingia rasmi katika tasnia ya filamu kwa kuandaa filamu ya kipekee itakayojulikana kwa jina X,  amesema kuwa filamu hiyo itaelezea maisha ya vijana wa Mazese na sehemu zingine ambazo kutokana na hali ya maisha kuwabana vijana wamejikuta wakiingia katika biashara haramu bila kujua madhara yake katika jamii.Alipoulizwa kuhusu kuwashirikisha wasanii nyota ambao amewashutumu kuwa wameishiwa na kutumia nafasi yao vibaya, amesema kuwa hana shaka na hilo kwa wale wasanii wa kazi atawatumia kwa kuwalipa na kufuata muswada wa filamu hiyo kama unavyotaka waigize, pia msanii huyo amesema muswada wa filamu hiyo umekamilika zoezi litakalofuatia ni kuanza.....

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging