Mwigizaji Nyota wa filamu Irene Uwoya anaamini kuwa uwepo wa tuzo katika tasnia ya filamu inaweza kuleta chachu kwa waigizaji na watayarishaji kwa ujumla jambo ambalo limekuwa halifanyiki kwa muda mrefu pamoja na kuwa na ongezeko la uzalishaji wa filamu kwa kiwango cha juu, mara nyingi kumekuwa na watayarishaji wa tuzo hizo lakini wamekuwa wakikumbana na vikwazo kutoka katika taasisi mbalimbali.“Uwepo wa tuzo katika tasnia ya filamu utaongeza ufanisi na ubora wa kazi zetu za filamu, Tuzo zitatufanya tufanye kazi nzuri zaidi ili kuingia katika ushindani, natoa wito kwa waigizaji wenzangu kufanya kazi kwa umakini ili kuleta msisimko na ushindani zaidi kwa waigizaji, watayarishaji na wadau wote katika tasnia ya filamu,” anasema Uwoya.Tuzo za filamu kwa mara ya kwanza ziliwahi kutolewa ziliitwa Risasi Awards mwaka 2005/2006 ukapita mwaka mwaka 2007/2008 zikaja tuzo za Vinara mwaka 2010/2011 Bora za 2010 zilizotolewa na mtandao mahiri wa habari za filamu wa filamucentral toka hapo hakuna tena tuzo kwa ajili ya tasnia ya filamu, hali ni tofauti na fani nyingine kama muziki
PRO24 RADIO/TV
CLICK AND ENJOY GOOD MUSIC
MIXTAPES
ARTIST PROFILES
Blog Archive
LOVE LINKS
PRO-24 DJS OFFICIAL BLOG
PRO24 ENTERPRISES. Powered by Blogger.