Mkali wa filamu nchini Nigeria na Afrika , Omotola Jalade anatalajia kuzindua filamu ya super star ya nyota wa filamu nchini Wema Sepetu, Jumapili katika Ukumbi wa Hoteli ya Giraffe Ocean View iliyopo Mbezi Beach .Filamu hiyo imechezwa na Wema ikionyesha maisha ya mtu maarufu na changamoto anazozipata ikiwemo kuandikwa mambo mbalimbali katika vyombo vya habari
Katika uzinguzi huo bendi ya Tanzania House Of Talent (THT) watatoa burudani kabla ya mashabiki kupata nafasi ya kupiga picha na msanii huyo . Omotola ambaye ni mke wa rubani Mathew Ekeinde ambao walifunga ndoa yao angani kwenye ndege atatoa nafasi ya kupiga picha na watu mbalimbali
Katika uzinduzi huo pamoja na burudani mbalimbali mashabiki watakaofika hapo watapata nafasi pia fursa ya kuiona filamu ya Super Star katika viwanja hivyo vya hoteli
Omotola ambaye yupo kwenye ndoa kwa miaka 16 akiwa na watoto wanne, ana jumla ya albamu mbili za muziki
Msanii huyo ambaye mwaka jana alitangaza kuachana na kucheza filamu kutokan na kuandikwa vibaya anatarajiwa kuwa kivutio kwenye uzinduzi huo ambao kiingilio kitakuwa sh. 30,000 kwa wakubwa watoto sh. 10,000








