Gwiji wa vipindi vya mahojiano vya terevisheni Oprah Winfrey ameanza kuingia katika tamaduni za pop linapokuja swala la watu kuwahoji .Kwa kawaida mwana dada huyo huwahoji waigizaji wakongwe, nyota wa muziki na wanamichezo kwa nia ya kuwapa watu ushawishi wa mafanikio ya maisha ,lakini mwana mama huyo amekiri kwamba kuwahoji waimbaji vijana wanotamba sana katika muziki wa pop kunalenga kuongeza idadi ya watazamaji wa shoo yake
Alisema “kwa miaka 25 nilijalibu kutofikiria idadi ya watazamaji ,nilifanya nilichofanya kwa sababu nilikuwa na mkataba ambao ulinipa uhuru wa kutohofia idadi ya watazamaji lakini hii ni biashara”
Kwa kuwahoji akinadada wa Kardashian na rap 50 Cent kumempa mafanikio Oprah kwa idadi iliyoongezeka ya watazamaji wa kipindi chake
Hivi sasa Oprah amemuanda nyota mwingine mkubwa Rihanna anayefuata kumhoji katika kipindi chake cha Oprahs ‘Next Chapter’ mahojiano
hayo yamepangwa kurushwa Agosti kwenye chaneli ya OWN Network








