Mama mzazi wa msanii wa filamu Elizabeth Michael 'Lulu' Lucresia Kalugila, amedai kitendo cha mwanawe kutamka mbele ya umma kwamba anaumri zaidi ya miaka 18, kililenga kuipa hadhi filamu yake Alidai pia kwamba mtoto huyo alifanya hivyo ili kuepuka unyanyapaa ambao ulikuwa ukifanywa dhidi yake na wasanii wenzake katika sanaa ya filamu wakimueleza kuwa ni mtoto Lucresia alidai hayo kupitia hati ya kiapo ya majibu aliyowasilisha Mahakama kuu kanda ya Dar es Salaam akikana mwanawe kuwa na umri wa zaidi ya miaka 18. Hati hiyo ya majibu iliwasilishwa jana Mahakamani hapo mbele ya Jaji Dk. Fauz Twaib na mawakili Kenneth Fungamtama, Peter Kibatala pamoja na Fulgence Massawe wanaomwakilisha Lulu Mawakili hao waliwasilisha hati hiyo ya majibu baada ya Jamhuri kuwasilisha ushahidi wa CD ya mahojiano ya Lulu na mtangazaji Zamaradi Mketema, maelezo yake aliyoyatoa polisi maombi ya hati ya kusafiria pamoja na leseni ya udereva Katika ushahidi huo wa jamhuri inaonekana muombaji wa kufanyiwa uchunguzi kuhusu utata wa umri wake akisema anaumri zaidi ya 18 Mama huyo amedai kwamba anaamini kuwa Lulu kutokana na utoto wake alitoa matamko ya uongo ili aweze kupata hati ya kusafiria na leseni ya udereva na kwamba si kweli amezaliwa Aprili 17, mwaka 1991 kama alivyoeleza.
KUONGOPA LULU MIAKA KULILENGA KUIPA HADHI FILAMU