Msanii anayetesa kwenye muziki wa kizazi kipya ‘Ben Pol’ amesema kuwa yupo mbioni kutoa video mpya itakayokwenda kwa jina la 'Maneno' Msanii huyo alidai kuwa anaamini video ya ngoma yake hiyo itafanya vizuri kwani anatumia muda wake mwingi na akili ili kuweza kutoa kitu tofauti
Alisema Video hiyo anaifanyia kampuni ya Karabani, ambayo itakuwa sokoni mwisho mwa mwezi huu
“Huu ndio mchakato ambao upo kwa sasa na naamini Mungu yupo karibu na mimi kwa sababu yeye ndio anayepanga hivyo tuombe mambo yaende sawa ili tuweze kuona matukio” alisema
Hata hivyo aliongezea kuwa baada ya mchakato huo kumalizika atakuwa kwenye kazi mpya ya kuwatungia nyimbo wasanii chipukizi ili nao waweze kufanya kama yeye au zaidi
"Tayari kuna msanii wa kike naanza naye anaitwa 'Female Ben Pol' ambaye nimefanya naye ngoma ambayo nayo itatoka mwishoni mwa mwezi huu" aliongeza