WANAMUZIKI wa muziki wa dansi nchini wanatarajia kufanya mkutano mkuu wa wanamuziki hao hivi karibuni kujadili masuala mbalimbali yanayoukabili muziki huo.Akizungumza Dar es Salaam jana, Msemaji wa kamati ya muda ya Wanamuziki hao Ally Choki alisema mkutano huo utajumuisha wanamuziki mbalimbali wa bendi za muziki huo na walio mikoani kuweza kujadili changamoto hizo.
"Tumeamua kulifanya hili makusudi kwa faida ya muziki wetu na hasa wanamuziki wachanga ambao wanachipukia katika muziki huo hivyo kwa wanamuziki waliopo mikoani ambao pia wanania ya kuhudhuria katika kikao hicho wafike ambapo tarehe halisi wataitangaza hivi karibuni," alisema.
Choki alisema muziki huo unakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na kususiwa na vyombo vya habari hivyo kuatarisha hali za wanamuziki kiuchumi hasa wanaochipukia.Alisema, wanamuziki wamekuwa wakivitegemea vyombo vya habari kwa kiasi kikubwa katika kuvipa sapoti ili waweze kupata mashabiki katika sehemu zao wanazotoa burudani na ndipo hapo wao wanaweza kuwalipa wasanii mishahara.
Naye Katibu wa muda wa kamati hiyo Khamis Dakota alisema, siku hiyo wataanika kila kitu kuhusiana na changamoto hizo kwani siku hiyo kutakuwa na wanamuziki wa bendi mbalimbali ambapo kila mmoja ataanika dukuduku lake.
"Tutazungumza kila kitu kwani sisi kama alivyotangulia kusema msemaji wetu tunakabiliwa na changamoto hivyo tukiwa wanamuziki wote ndio italeta mantiki kubwa kwani hakuna mtu atakayeweza kumsemea mwenzake," alisema.
PRO24 RADIO/TV
CLICK AND ENJOY GOOD MUSIC
MIXTAPES
ARTIST PROFILES
Blog Archive
LOVE LINKS
PRO-24 DJS OFFICIAL BLOG
PRO24 ENTERPRISES. Powered by Blogger.