Jaqueline Wolper Massawe ‘Jack’ anasema kuwa suala la mavazi mara nyingi utegemea tukio au sehemu husika tofauti na watu wanavyofikiria kuwa unapomwona msanii huyo katika mavazi fulani ndio wanajua ni mavazi yake halisi, na kulalamika kama wasanii ndio wanaovaa vibaya katika jamii Mara nyingi mavazi yanategemea sana sehemu husika hata nikiwa (Star) Nyota siwezi labda kwenda kanisa nimevaa kimini na sehemu ambazo hazistaili kwa mavazi yaliyo tofauti bali nitavaa vazi linalostahili, lakini kwa bahati mbaya lawama inatuangukia sisi wasanii tukionekana kama ndio tunaovaa vibaya,”anasema Jack.
Aidha amesema kuwa inakuwa vigumu mtu ukienda sehemu kama Disco hauwezi kuvaa sehemu nyingine isiyohusika, lakini pia amesema kuwa kuna nguo zinavaliwa katika filamu tu na mtu hawezi kuvaa mtaani, pamoja na kuwaangalia sana wasanii lakini pia wasanii nao ni sehemu ya jamii jambo ambalo inatakiwa pia watu walione hilo kwani kuna watu si wasanii na wana viwalo vya ajabu...