Google PlusRSS FeedEmail

WASANII WAIPONGEZA BAJETI YA SERIKALI



SIKU chache baada ya serikali kuwasilisha bajeti ya mwaka wa fedha 2012/2013,bungeni mjini Dodoma baadhi ya wasanii wameipongeza serikali kwa kuweza kutambua mchango wa kazi zao kwa kuwaingiza katika mfumo rasimi utakaolinda kazi zao

Wasanii hao wameipongeza serikali kwa jitihada za kuinua uchumi wa nchi na kipato cha msanii kwa kulinda kazi za wasanii kupitia mapato yatakayopatikana

Akizungumza Dar es Salaam leo Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF) Bw. Simon Mwakifwamba alisema kuwa, mfumo wa sekta rasmi utapunguza wizi wa kazi za wasanii pamoja na kulinda haki ya msanii

“Kutakuwa na takwimu sahihi za mauzo ya kazi za wasanii na mapato ya wasanii pia yataeleweka na mwisho wa mwaka unaweza kujua nani ameuza kwa kiwango gani” alisema

Pamoja na hayo alisema kuwa watakuwa na kila sababu ya kudai serikali kwani kila kitu kitakuwa kipo wazi hivyo serikali itoe elimu kwa jamii ili kujua kazi ipi ni sahihi kununua kwa ajili ya kuongezea pato la taifa

Aliongezea kwanba wanyonyaji wanauchukia mfumo huo kwani walishazoea kuwakandamiza wasanii hivyo mfumo huu ni tiba kwa wale wote waliozoea kujinufaisha kwa kupitia nguvu za wasanii

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging