UPELELEZI BADO KESI YA LULU
Upande wa Jamhuri katika kesi ya muigizaji wa Filamu nchini , Elizabeth Michael maarufu kama Lulu anayekabiliwa na kesi ya mauaji umedai kuwa upelelezi wa shauri hilo bado haujakamilika .
Jana wakili wa seriakli Keneth Sekwao aliyaeleza hayo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Augustina Mmbando wakati kesi hiyo ilipokuja kuatajwa. Lulu anakabiliwa na kesi ya mauaji ya msanii mwenzake Steven Kanumba katika mahakama hiyo
Kutokana na hali hiyo kesi imeahirishwa hadi Julai 2 mwaka huu itakapoletwa tena kutajwa,Hata hivyo jana Lulu hakupandishwa kizimbani na badala yake aliwakilishwa na wakili Peter Kibatala ambaye ni miongoni mwa mawakili wanaomtetea katika kesi hiyo
Juni 25 mwaka huu Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam inatarajia kutoa uamuzi wa kuhusu maombi ya upande wa utetezi katika kesi hiyo kuhusu umri wa mshitakiwa huyo