Google PlusRSS FeedEmail

WAZEE WAIPOKEA FILAMU YA MWALIMU NYERERE

Filamu ya Mwalimu Nyerere iliyoingia sokoni hivi karibuni kwa usambazaji wa Kampuni ya Steps, imepokelewa kwa shangwe na wazee ambao ndiyo wameonekana kuinunua kwa wingi...Katika filamu hiyo kunaelezea mambo mbalimbali yaliyowahi kufanywa na Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere imetengenezwa na muigizaji wa sauti za watu maarufu nchini Steven Mengele 'Steve Nyerere'


Akizungumza Dar es Salaam jana, Steve Nyerere alisema katika tathimini ya muda mfupi aliyoifanya tangu filamu hiyo kuingiza sokoni, idadi kubwa ya watu wa rika la kati na wazee wameonekana kuinunua na kuipenda zaidi filamu hiyo.Alisema kwa upande wa mikoani filamu hio imepokewa kwa mapenzi makubwa na kwamba kila mtu anatamani kuiona kutokana na ukweli kwamba ameweza kuvaa uhusika wa Mwalimu Nyerere jambo lililowavutia wazee na watu wa rika la kati


Mwigizaji huyo alisema katika muda mfupi wa filamu hiyo kuingia sokoni amekuwa akipata maoni mbalimbali hasa ya pongezi kwa watu kutoka katika mikoa mbalimbali ya Tanzania wakionekana kuvutiwa na uhusika aliouvaa kupitia filamu hiyo..Alisema filamu hiyo ameitengeneza katika kijiji cha Butiama ambacho ndicho alichokuwa akiishi Nyerere na kwamba ameshirikiana vyema na watu wa Butiama pamoja na mke wa Mwalimu , Mama Maria Nyerere


Alisema kutokana na muitikio mzuri wa filamu hiyo, anajipanga kutoa nyingine ambayo ataitangaza mara tu baada ya kukamilika na anaamini itawavutia watu wengi hasa kutokana na jinsi atakavyoicheza..Kabla ya filamu ya Mwalimu Nyerere, Steve alitamba na filamu ya Mr. President ambayo alisema ni zawadi kwa Rais Jakaya Kikwete katika kuadhimisha miaka 50 ya Uhuru wa Tanganyika

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging