MSANII maarufu kwenye tasnia ya filamu na maigizo nchini Rashid Nassor 'Chid Mzee wa Mbele' amesema kuwa yuko mbioni kutoa filamu ya mapenzi itakayoitwa Bimu..Akizungumza Dar es Salaam msanii huyo alisema katika filamu hiyo itakayoitwa 'Bimu'atamshirikisha nyota wa muziki wa kizazi kipya Ali Kiba..
"Katika filamu hiyo mpya nitacheza kama mtu aliyezaliwa katika familia ya kitajiri nikiwa na msanii mwenzangu aitwaye Back Boban" alisema Chid..Alisema msanii Ali Kiba yeye atakuwa mtu wa kunyanyasika, lakini atampata mama mtu mzima ambaye atakuwa anamtunza Msanii huyo alisema ameamua kucheza filamu hiyo kutokana na kundi lake la Bongo Dar es Salaam kushindwa kuendelea kurusha vipindi vyake kwenye luninga ..Chid alisema kuwa baada ya kusua sua kwa kutoonekana kurushwa hewani igizo la Bongo Dar es Salaam ambapo wadau walikuwa wakiogopa kumshirikisha katika filamu zao..