Google PlusRSS FeedEmail

ZIFF KUJA NA WARSHA NA KONGAMANO

Waandaaji wa tamasha la filamu la Zanzibar International Film Festival (ZIFF) wameandaa warsha na kongamano kwa wameandaa na watayarishaji wa filamu.Warsha hiyo itaanza Julai 9 mwaka huu na kushirikisha watayarishaji na waandaji kutoka nchi mbalimbali , zitakazo shiriki tamasha hilo linalofanyika kila mwaka Ngome Kongwe Zanzibar Akizungumza Dar es Salaam jana Mratibu wa tamasha hilo, Martine Mhando alisema warsha hizo zitasaidia kuongeza ujuzi katika kupiga picha na kuhariri filamu Alisema pia kutakuwa na warsha maalum ya uongozaji itakayotolewa na Mario Van ambaye ni muongozaji wa filamu wa kimataifa ambapo itawasaidia zaidi waongozaji wa filamu hapa nchinib Mhando alisema tamasha hilo kwa mwaka huu litawavutia zaidi washiriki kutokana na ZIFF kujipanga na kufanya mabadiliko makubwa mwaka hadi mwaka , mbali na warsha hiyo tamasha hilo pia linatoa nafasi kwa wasanii wa filamu kutoka nchi mbalimbali kwa kazi zao kuingia kwenye tuzo za ZIFF ambazo zinatolewa kwa msanii aliyefanya vizuri katika tuzo ya filamu bora , msanii bora na tuzo nyinginezo.....

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging