Kituo cha televisheni cha East Africa (EATV) kimeanda shindano la kutafuta kundi bora la kucheza muziki kwa mkoa wa Dar es Salaam ambapo washindi watatwaa zawadi ya pesa taslim kiasi cha sh.milioni 5 Shindano hilo litafahamika kwa jina la ‘Dance Mia Mia’ ambapo walengwa ni wale wote wenye uwezo wa kucheza aina yoyote ya muziki wenye umri wa kuanzia miak 14 hadi 90 Imefafanuliwa zaidi kuwa mtu ambaye atashiriki katika mchakato wa kutafuta kundi bora la kucheza jijini Dar es Salaam atatakiwa kuwa kwenye kundi lenye watu wane hadi sita Mchakato huo utakuwa utakuwa na mchujo wa awamu tofauti hadi fainali ambapo kundi litakalo ibuka kidedea ndilo litatwa taji la kundi bora la kucheza mkoa wa Dar es Salaam na pia kupata kitita cha sh. Milioni 5 Makundi tofauti ya kucheza kutoka wilaya zote tatu za Dar es Salaam yanatakiwa kujitokeza kushiriki katika mchakato huo ambao hatua za awali zinaanza ijumaa
PRO24 RADIO/TV
CLICK AND ENJOY GOOD MUSIC
MIXTAPES
ARTIST PROFILES
Blog Archive
LOVE LINKS
PRO-24 DJS OFFICIAL BLOG
PRO24 ENTERPRISES. Powered by Blogger.