Ikiwa ni takribani wiki moja tangu adondoke jukwaani mwanamuziki Adele ambaye ni mjamzito ametajwa kuwa mingoni mwa watu mashuhuru wanaopata fedha nyingi ulimwenguni , kwa mujibu wa gazeti la The Sun mwanadada huyo ni miongoni mwa watu mashuhuri 30 wanaoingiza kipato kikubwa
Likinukuu jarida la Forbes mwanamuziki huyo amekadiliwa kuwa pato la pauni milioni 23 ambalo aliliingiza kupitia mauzo ya kazi yake ya muziki kuanzia Mei 2011 hadi Mei 2012. Kwa kipidi hicho mwanamuziki huyo atakuwa akishika nafasi sita kati ya wanawake wenye nazo ambao wanaongozwa na Taylor mwenye utajiri wa pauni milioni 37 ambaye atafuatwa na wanamuziki wengine waliopo kwenye orodha ya vinara watano Justin Bieber, Rihanna, Lady Gaga na Katy Perry








