JUNIOR KUJIUNGA NA BENDI MPYA KATIKATI YA MFUNGO
Mkali wa kwenye anga za muziki wa dansi nchini Kalala Junior amesema kuwa atawaeleza washabiki wake kuhusiana na bendi ipi atajiunga nayo katikati ya mfungo wa mwezi mtukufu wa ramadhani, akizungumza jijini mwisho wa wiki alisema kuwa ameamua kujipimzisha na maswala ya muziki kutokana kuchoshwa na kazi hiyo.
Muimbaji huyo alieleza msimamo wake huo alipotakiwa kujibu swali kuhusu bendi ipi aliyotarajia kujiunga nayo baada ya kujiengua Mapacha Watatu.Kalala alijitangaza kujitoa mapacha watatu wiki kadhaa zilizopita bila kuweka wazi kuhusu mipango yake ya baadaye, ingawa kulikuwa na uvumi kuwa atajiunga na bendi ya mashujaa
Akizungumzia tetesi hizo Kalala ambaye ni mtoto wa jabari wa muziki wa dansi nchini Hamza Kalala amefunguka na kukielezea chanzo kimoja cha habari kuwa, hadi sasa bado hajaamua kujiunga na bendi yoyote
“Nimeamua kupumzika kwa miezi miwili lakini ifikapo katikati ya mwezi Ramadhani nitaweka wazi kuhusu bendi ipi nitajiunga nayo”alisema
Aliongezea kuwa kama binadamu amefanya kazi ya kuimba kwa muda mrefu na kukesha kwenye kumbi za burudani kwa saa nyingi hivyo anahitaji kupumzika, hata hivyo Kalala alikiri kuwa amekuwa akifuatwa na bendi nyingi zikimtaka ajiunge nazo lakini bado anatafakari kuhusu ipi itakayomfaa zaidi








