Mwandishi wa muswada Ali Yakuti ameshutumiwa kwa kumdhulumu mwigizaji wa filamu hapa nchini Godliver Godian ‘Nancy’ malipo hayo yanatokana na ushiriki wa filamu ya Who is the Looser , filamu hiyo iliandaliwa na mwandishi huyo na kwenda kurekodiwa nje ya Jiji huko Kibaha, msanii huyo akiongea kwa uchungu amesema kuwa Yakuti ametumia nafasi ya kujuana kumdhulumu haki yake.
Ali Yakuti mtunzi na mwandishi wa muswada akiwa na Irene Paul.
“Naamini karibu washiriki wote wa filamu ya Yakuti wamelipwa lakini kwangu imekuwa shida, ukimpigia simu hapokei, lakini jambo la pili baya kushinda yote na hilo linanifanya roho iume zaidi ni jinsi nilivyojitoa katika filamu hiyo na kujikuta nikifanya kazi nyingine tofauti na ile ya kuigiza, najiuliza kwanini hataki kunilipa fedha ambayo ni jasho langu?,”anasema Nancy.Nice amesema kuwa wakati filamu hiyo ikirekodiwa hakukuwa na mtu wa mapambo (Make up) kazi ambayo aliifanya kwa ajili ya kuifanya kazi hiyo iwe bora lakini hakupata malipo stahili na sasa hapokei siku yake tena, pia amesema kuwa hivi karibuni Yakuti alimpigia simu jambo ambalo hata yeye alishangaa kwa kutaka kurudia vipande vya filamu hiyo naye aliulizia kuhusu malipo akamtajia siku ya kurudia vipande hivyo, lakini siku ilipofika Yakuti hakupokea Simu.
.
Nancy akiwa katika pozi la picha.
“Unajua mimi niliacha kazi kwa ajili ya kurekodi kazi yake kwa sababu pamoja na kusomea fani nyingine lakini napenda sana kuigiza, nimekaa Kibaha zaidi ya wiki alafu mtu bila huruma anakudhulumu jasho lako hakupi hata senti tano! Inauma sana,”anasisitiza Nancy.
KWA HISANI YA FC