Pazia la mchujo wa kusaka vipaji vya wawakilishi wa mkoa wa Arusha katika fainali za EBSS 2012 lilifungwa rasmi juzi katika ukumbi wa Triple A mjini hapa na sasa kazi inahamia jijini Mwanza jumamosi
Siku mbili za ushindani mkali ulioleta zaidi ya vijana mia 800 kugombea nafasi ya kuiwakilisha Arusha zilikuwa ngumu kwa majaji kuamua wangapi watawaacha na wengine kuwachukua , pamoja na vijana wengi wa mjii huo kupenda kuimba nyimbo za Hip Pop zikisifika zaidi kuwatoa wasanii hao katika shindalo hilo ilikuwa ni tofauti kwa wasanii wengi kuamua kuimba Jaji mkuu wa EBSS alikkiri kuwa katika mikoa ya Lindi Dodoma na Kisiwa cha Zanzibar ambapo walikwenda kusaka vipaji ila kwa Arusha hali ilikuwa nzuri zaidi ya mikoa hiyo