Google PlusRSS FeedEmail

USHER RAYMOND: MWANAMUZIKI MWENYE VIPAJI LUKUKI

Usher Raymond msanii mwenye sifa kemkem ikiwemo ya uandishi wa nyimbo, uimbaji, uigizaji,mchezashoo mwanamitindo, utayarishaji, mbunifu,pamoja na kuwa mfanyabiashara .Nyota huyo aliyezaliwa miaka 32 huko nchini Marekani alianza kushika chati kwenye miaka ya 1990 alipotoa albamu yake ya pili iliyotambulika kwa jina la ‘My Way’ ndani ya albamu hiyo kuna kibao cha ‘Nice and Slow’ kilichoshika namba moja katika chati ya Billboard Hot 100, katika tasinia ya muziki Usher ametamba vilivyo kutokana na kuwa kwenye muda mrefu katika burudani
Mwanamuziki huyu amechangia kwa kiasi kikubwa kugundulika kwa kipaji cha kijana Justin ,pamoja na hayo muziki umechangia kwa kupata tuzo nyingi zikiwemo tuzo za Albamu bora ya soul , muimbaji bora wa kiume wa soul/R&B, muimbaji bora wa Pop/Rock na mwimbaji bora wa mwaka
Akizungumzia maswala ya fedha Usher mpaka sasa anamiliki utajili unaofika dola milioni 32 (sh bilioni 45)Usher anaishi maeneo ya Alpharetta, Georgia katika jumba lenye vyumba vitano vya kulala na vine vya kuogea, jumba hilo lilinunuliwa kwa dola milioni 2.3(sh bilioni 3.2) akilisifia kwa kuwa na uwanja mkubwa wa mazoezi na sehemu ya kuchezea muziki wa kisasa ,pamoja na hayo jumba hilo la kifahari lina sifa ya kuwa na saluni, bwala la kuogelea, nyumba ya wageni pamoja na studio za kutengenezea muziki
Jumba hilo ndilo alilofanyia harusi yake ya kifahari na aliyekuwa mwenza wake Tameka Foster,kama ilivyo kwa wasanii na watu wengine msanii huyo ametumia kiasi cha dola 300,000(sh milioni 420)kwa ajili ya kununua gari la kifahari aina ya chauffeur.ukiachilia maswala ya muziki Usher amekuwa akijihusisha na uigizaji wa filamu na hadi sasa anapotamba na ‘The Killers’iliyotoka Aprili 6, 2010 tayari ameshatoa jumla ya filamu tisa . Usher alifunga ndoa na aliyekuwa mpenzi wake Tameka, Agosti 3, 2007 na kufuatiwa na sherehe iliyofanywa kuwa siri , wanandoa hawo walibahatika kupata watoto wawili , Juni 29 wanandoa hao walitengana baada ya kukaa mbalimbali karibu mwaka mmoja Usher na Alicia Keys wamekuwa wakihusishwa na mahusiano ya mapenzi wakati waliposhirikiana kupiga shoo ya wimbo ‘My Boo’

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging