Google PlusRSS FeedEmail

DOGO RAMA AIBUKA MSHINDI WA NANI MKALI




Muimbaji wa bendi ya African Stars ‘Twanga Pepeta’Ramadhani Athumani ‘Dogo Rama’ ameibuka mshindi wa mashindano ya nani mkali kwa wanamuziki wa muziki wa dansi yaliyomalizika wiki iliyopita na kujinyakulia kitita cha sh. Milioni moja.

Dogo alipata kula zaidi ya 8000,kutoka kwa mashabaki wake na kuwaburuza wapinzani wake sita kutoka katika bendi za Twanga pepeta ambayo iliyotoa wanamuziki wawili, K Mondo Sound, Mashujaa, Extra Bongo na Diamond Musica.

Nafasi ya pili katika mashindano hayo ya kuwania kitita cha sh. 1,000,000 pamoja na kurekodiwa muziki na video zao binafsi ilichukuliwa na Passya wa Mashujaa , nafasi ya tatu ilikwenda kwa Venus pia wa Twanga pepeta, Akizungumzia ushindi wake Dogo Rama alisema hakuamini kama angeshinda katika mashindano hayo, licha ya kupewa moyo mara kwa maraa na mashabiki wake ambao walimpigia kura na kuweza kushinda

“Mchakato ulikuwa mgumu hasa siku ya fainali kwani ulikuwa unaokota karatasi na wimbo utakaukuta ndiyo unatakiwa kuimba lakini namshukuru mungu,ingawa nilikutana na nyimbo za wanamuziki wakongwe wa Congo, Pepe kale na Defao lakini nilimudu kuimba nyimbo zao na kuwavutia mashabiki walioudhuria na majaji” alisema

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging