MASHUJAA KUTAMBULISHA KAZI MPYA
Rais wa bendi ya Mashujaa ‘Wanakibega’Charles Gabriel ‘Chalz Baba’ amewataka wapenzi wa muziki nchini waipokee kazi yao mpya itakayozinduliwa hivi karibuni .
Akizungumza jijini Dar es Salaam hivi karibuni wakati wakitambulisha video yao mpya ya Risasi Kidole Chalz Baba alisema kuwa wamejipanga vizuri kwa kuanza na kazi hiyo ya Risasi Kidole ambayo imeshakamilika.
Alisema kuwa teyari wameshafyatua video mpya ya wimbo huo ambayo itazinduliwa baada ya mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani , aliongezea kuwa kuna baadhi ya watu wanadai kuwa wanaenda kwenye bendi hiyo kama kutalii wakiwa hawajui nini kinachoendelea
“Sisi tumekuja kazini nia yetu ni kuleta burudani lakini kunawatu walikuwa wanasema kuwa sisi tumekuja kucheza sasa ndio wataona tunafanya nini kwa kuanza na kazi hii ya kwanza “ alitamba muimbaji huyo
Meneja wa bendi hiyo Martin Sospeter alisema video hiyo itaanza kuonekana kwenye vituo mbalimbali vya televisheni nchini kote wakati wowote kuanzia sasa , aliongezea kuwa licha ya kutoa wimbo kuna nyimbo nyingine teyari zimeshakamilika na zinatarajia kutoka hivi karibuni
Sospeter alisema kuwa hapo awali walikuwa wamepanga kufanya utambulisho wa wimbo huo lakini wameamua kusogeza mbele ili hata waislamu waweze kushuhudia utambulisho huo
Licha ya kuzungumzia wimbo huyo Sospeter alisema kuwa katika kipindi cha mwezi mtukufu wa Ramadhani bendi hiyo itakuwa inafanya burudani kama kawaida isipokuwa siku ya jumatano








