Bendi ya muziki wa dansi ya Extra Bongo, inatarajiwa kufanya onesho maalumu kwa ajili ya kuwaaga wapenzi wao, kabla ya ziara yao ya Ulaya, kwenye ukumbi wao wa Bongo Resorts zamani New Write House uliopo Kimara jijini Dar es Salaam, kesho.Onesho hilo litapambwa na wakali wa Bongo fleva kama, Chid Benzi, Matonya, Hussein Machozi na Q Chillah, sambamba na burudani kutoka katika bendi hiyo.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Extra Bongo, Ally Choki, alisema, wamepata mkataba wa kushiriki tamasha la Kampuni ya First Africa iliyopo nchini Finland, ambako wanategemea kuondoka Jumapili alfajiri.“Tamasha hili ambalo ni la kila mwaka, linatarajiwa kuanza Julai 18, na katika bendi yetu tutaondoka watu 15 pamoja na Mfadhili wetu, Chief Kiumbe na tutapata nafasi ya kufanya shoo katika nchi mbalimbali kama, Norway, Sweden na Holland, ‘Uholanzi’,” alisema Choki.
Choki aliwataja watakaokuwamo katika safari hiyo kuwa ni yeye mwenyewe kama Mkurugenzi, Rogate Hegga ‘Caterpillar’ kiongozi wa msafara huo, Athanas Michael, Emmanuel Kisa ‘Bob Kisa’ na Ramadhan Mohoza ‘Pentagon’ wakiwa ni waimbaji.Kwa upande wa wapiga vyombo ni Martin Kibosho, Hosea Mgonahachi, Adam Hassan, Tom Migula na Salum Issa ‘Chakuku’ huku wachezaji wakiwa ni Mussa Hassan ‘Nyamwela’, Isaac Buruhan, Otilia Boniface, Angela Joshua na Zawadi.Choki aliongeza kuwa, kwakuwa watu wanaoondoka ni wengi kuliko wanaobaki, wanaomba radhi kwa wapenzi wao kwa kutofanya maonesho yao kwa kipindi hicho ambacho watakuwa safarini.