Kinara wa filamu kutoka Hollywood mwenye asili ya Mexico, Mario Van Peebles `MVP', leo anatarajia kuwa na wakati maalum na watoto wapenzi wa filamu nchini ambapo atapiga nao picha, kusaini vitabu vyao vya kumbukumbu na kujibu baadhi ya maswali yao.
Hii itakuwa ni siku yake ya pili baada ya jana kuzindua filamu yake inayojulikana kwa jina la We The Party kesho katika ukumbi wa New century Cinema uliopo katika ukumbi wa Mlimani City.
Mario ambaye pia ni mwandishi, muongozaji na muigizaji, amewasili nchini akiwa na mwanaye anayeitwa Mandela Van Peebles ambaye ndio kinara katika filamu hiyo na meneja wake Michael Cohen ambapo pamoja na mambo mengine pia amekuja kushiriki katika tamasha la filamu la nchi za majahazi.
Moja kati ya filamu zinasotamba alizowahi kuigiza na kuongoza ni tamthilia ya Lost ambayo inatajwa kwamba iliwahi kuongoza kwa kuangaliwa ukilinganisha na tamthilia za Prison Break na 24, ambapo katika tamthilia hii alionekana kama Dk Linus.
Filamu jingine ambazo ziliwahi kutamba ambazo ameigiza ni pamoja na Exterminator ya mwaka 1984, New jack City (1991), Full Eclipse(1992), Solo(1996), na All things Fall Apart(2011) ambayo iliwahi kuleta utata baada ya mwandishi Chinua Achebe kutoka Nigeria kutaka kuifungia akidai maudhui yake yanahusisha kitabu chake kilichowahi kutumika kwenye mtaala wa shule za sekondari nchini.
Akiongea na Mwananchi mwenyeji wa staa huyo ambaye pia ni mratibu wa Tamasha la filamu zanzibar ZIFF, Ibrahim Mitawi amesema Mario atatumia wikiendi nzima jijini Dar ambapo atakuwa akikutana na mashabiki wake na kufanya shughuli mbili tatu za kijamii.Filamu ya We the Party inaelezea jinsi sherehe ambavyo haiwezi kufanyika bila washerehekeaji hivyo ujumbe mkubwa uliobebwa humo ni kwamba usiulize wapi kuna sherehe, bali wewe mwenyewe ndio sherehe hivyo sherehe inaweza kuwa popote pale penye watu.Filamu hiyo inatarajiwa kuoneshwa kwa wiki nzima.
Huyu anakuwa ni staa wa kwanza kutoka Hollywood kuzindua filamu yake nchini huku akiwa wazi kwa mashabiki wake.
KWA HISANI YA MDIMU