Google PlusRSS FeedEmail

FILAMU YA LAURA YAMTESA CHUCHU HANS

                     
Mwigizaji mahiri wa filamu Chuchu Hans amesema kuwa toka aanze kuigiza hajawahi kuigiza sehemu ngumu katika filamu kama aliyoigiza katika filamu ya Laura akiongea kwa unyonge alisema kuwa pamoja kuwa yeye ni binti wa Kiislamu lakini alilazimika kuingia katika sanduku la kuzikia akiwa kama mtu aliyefariki na kuagwa kwake ilikuwa ni mtihani. “Filamu ya Laura kwangu ilikuwa mtihani kweli maana nimeigiza kama wa mtoto Laura na kufariki kimaigizo siyo kabisa, unajua kwa nini ilikuwa mtihani kwangu kwa sababu pia huyo mtoto Laura ni mwanangu kweli ambaye nimemzaa mwenyewe kuna wakati nikawa nafikiria mwanangu atakuwa katika hali gani? Lakini kwa sababu ni kazi haikuwa na jinsi,”anasema Chuchu.Chuchu anasema kuwa anajivunia kuigiza vizuri akiwa na mtoto wake kwani hadi sasa msanii huyo ambaye ni mwanaye anaigiza vizuri na kujikuta akiwa msanii wa kutegememewa kwani kwa sasa mtoto wake anashiriki filamu nyingi kwa kila aliyebahatika kumwona anahitaji kumtumia katika filamu yake anayoandaa Chuchu kwake ni faraja.

Filamu ya Laura imetengenezwa na kuongozwa Suleiman Barufu mtayarishaji wa filamu anayefanya vizuri katika tasnia ya filamu Swahiliwood katika filamu hiyo pia ameshiriki Stanley Msungu ‘Seneta’ Barafu mwenyewe pamoja na wasanii wengine wakali wanaotesa katika tasnia ya filamu.

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging