Msanii mahiri katika tasnia ya filamu Nchini Mohamed Fungafunga ‘Mzee Jengua’ amesema kuwa wasanii wengi wamejikuta wakidhulumiwa au kupata malipo madogo kutokana na kazi ya uigizaji kutokana na kuwa na uelewa mdogo katika kuingia mikataba na baadhi ya watayarishaji wa filamu hapa nchini, Mzee Jengua amesema baada ya kuligundua hilo yeye ameamua kumtafuta meneja wake ambaye atakuwa akipatana na kufuatilia kila kitu na kumweleza aigize katika filamu husika kama inamlipa kutokana na ushauri wa meneja wake.“Wasanii wengi tuna matatizo katika uelewa, kutokana na hilo tunajikuta tukifanya kazi nyingi kwa ujira mdogo ambao kupiga hatua inakuwa kazi kuna baadhi ya waandaaji akitaka kukudhulumu au tuseme kukubaisha anakuletea mkataba labda umeandikwa kwa lugha ya kigeni na hakupi nafasi hata ya kwenda kujiuliza kwa mwanasheria au mtu mwenye uelewa na utaalamu wa mambo ya mikataba, ukiangalia na wewe unahitaji hiyo fedha basi unaingia mkenge,”anasema Mzee Jengua.
Katika kukabiliana na hali hiyo msanii huyo ameamua kuingia mkataba na meneja wa kusimamia kazi zake zote kwa mantiki hiyo mtayarishaji yoyote atawasiliana na meneja wake ili kuepuka matatizo na usumbufu ambao unaweza kutokea katika utendeji wa kazi hizo, Mzee Jengue ni moja kati ya wasanii wakongwe waliotamba sana katika michezo ya maigizo siku za nyuma iliyokuwa ikirushwa katika kituo cha Televisheni cha ITV akiwa na kundi la Kidedea.