Alex Chalamila ‘Mack Reagan’ anasema katika kundi lao kila siku ni kazi, kwa hiyo inampasa kila msanii kuumiza kichwa kwa ajili ya kukaa juu bila kushuka kwani kundi lao ni kundi la kazi, lakini kwake anachojivunia ni kuwa na ubunifu wa kubuni maneno na kuwa maarufu mitaani lakini hata baadhi ya watu maarufu kuitumia kwake ni faraja.“Unajua ukiwa Komedi Orijino ni kazi kwenda mbele na kila msanii unayemuona yupo safi na ana ubunifu wake, kwa sababu tunajua kuwa tuna watazamaji wengi ambao wanahitaji huduma yetu ili waburudike kila wanapotaza kipindi chetu na mimi nipo kwa ajili ya kuwa kuwachangamsha,”anasema Mac Reagan Mack Reagan amekuwa akijizolea umaarufu kwa aina ya staili zake ambazo kweli utamba mitaani na kutumika kwa kila msanii na kutawala misemo hiyo, kama Shemejiii, Why kwanini? Na misemo mingine Mack Reagan anaunda kundi la Komedi Orijino akiwa na Joti, Masanja Mkandamizaji, Mpoki, Wakuvanga pamoja na Vengu anayeumwa.
PRO24 RADIO/TV
CLICK AND ENJOY GOOD MUSIC
MIXTAPES
ARTIST PROFILES
Blog Archive
LOVE LINKS
PRO-24 DJS OFFICIAL BLOG
PRO24 ENTERPRISES. Powered by Blogger.








