Pichani kati ni Mwanamuziki mahiri Josee Mara akifafanua kuhusiana na mikakati yao waliyonayo kwa sasa mara baada ya mwanamuziki mwenzao mmoja,Kalala Jr kutimka na kuwaacha wakiwa wawili badala ya watatu. Josee Mara amesema wao wako fiti na hakuna kilichoharibika,kwani kuna wanamuziki wengine kadhaa ambao ni wazuri na watafanya nao kazi kama ilivyokuwa kwa Kalala Jr."Na sasa hivi nakuhakikishia Da'Suzzy tutapiga kazi ile mbaya, kwa sababu hao vijana tunaowaongeza ni wanamuziki wazuri na tunawahamu toka kitambo, kwa hivyo naamini mambo yatakuwa sawa na washabiki wetu wasivunjike moyo,waendelee kutuunga mkono tu,sisi ni wapambanaji kwa hiyo ni lazima tupambane"amesema Josee Mara. Aidha Khalid Chokoraa ameongeza kuwa katika kuonesha bado wako fiti wamekwisharekodi singo yao moja iitwayo ONA NAONEWA, ambayo wataitambulisha hivi karibuni kwa mashabiki wa muziki wa dansi
MAPACHA BILA KALALA, BADO NGANGARI