Google PlusRSS FeedEmail

MIMI SI MKATA VIUNO VYA BURE – SHILOLE .

Mwanadada mwigizaji na mwanamuziki Zuwena Mohamed ‘Shilole’ amesema kuwa baada ya kujiongezea fani nyingine ya uimbaji na kufanya vizuri ni kama kafungua njia kila mwigizaji wa kike anataka kuimba japo hawana uwezo huo, anasema kuwa wanapoona Shilole anakataa viuno wanajua kuwa kila msanii atakata viuno tu na kuwa mwanamuziki mkali.“Nawapa pole wenzangu toka nimefungua njia na kuanza kuimba naona watu wanakurupuka na kuingia katika fani ya uimbaji, sikukurupuka nilijipanga kwa ajili ya kazi na kazi inaonekana napata show ambazo hata wasanii wakubwa hawapati, mimi si kama hawa wakataa viuno wanaoiga tu baada ya kumuona Shilole sifanyi maigizo nafanya kazi inayokubaliki katika jamii,”anasema Shilole

Dongo hilo la Shilole linaonekana kuwalenga wasanii wenzake wa filamu ambao nao pia wameamua kuingia katika tasnia ya uimbaji kwa kasi, Shilole anasema kuwa muziki na filamu vinampatia kipato na kuweza kuwasomesha watoto wake wawili katika shule ya kimataifa, anaendesha gari nzuri, anaishi nyumba nzuri kwake filamu na muziki ni biashara, pia Shilole amekamilisha nyimbo zake nyingine alizowashirikisha wasanii Mzee Yusuf (Kachumbari), Barnaba (Surprise), Q Chilla (Dudu) na wimbo wa Viuno alioshirikisha wasanii Richi Mavoko na Kitokololo.Shilole anasema na ana kampuni yake anayoiita Shilole Classic ndio inayosimamamia kazi zake zote ikiwa muziki na filamu.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging