Nasir Jones (amezaliwa Septemba 14, 1973 ni mwanamuziki rap na mwigizaji kutoka nchini Marekani.Anafahamika zaidi kwa jina lake kisanii kama Nas. Zamani alikuwa akijiita . Nas ni mtoto wa mwanamuziki wa jazz wa zamani Mzee Olu Dara.
Alizaliwa na kukulia katika nyumba za miradi za mjini (nyumba za watu wenye kipato cha chini) Queensbridge, New York.Nas alisaini mkataba na studio ya Columbia Records mnamo mwaka wa 1994, na kutoa albamu yake ya kwanza ya 'Illmatic'. Albamu ya 'Illmatic' ilipata kuwa bora na kufahamika zaidi na mauzo bora.
Baadaye albamu kadhaa za Nas zilifuata. Albamu hizo ni pamoja na It Was Written ya 1996, I Am... and Nastradamus ya 1999, na Stillmatic ya 2001. Nas alikuwa mmoja kati ya wanaounda kundi la muziki wa rap na hip hop lililofahamika kama 'The Firm', ambalo limejumlisha wasanii wengine kama vile AZ, Foxy Brown, na Nature. Ingawa, kundi halikufanya kazi nyingi na badala yake wakatoa albamu moja tu ya pamoja.
Kuanzia mwaka 2001 hadi`2005, Nas aliusishwa katika ugomvi mkubwa na rapa mwenziwe Jay-Z. Marapa wote walikuwa wakishambuliana kwa kutumia nyimbo zao.Wawili hao ugomvi wao ukaja kwisha baada ya kualikwa katika tamsha la muziki la New York City-area hip-hop za vituo vya redio.
Nas akasaini mkataba na studio ya Jay-Z maarufu kama Def Jam mwaka 2006.Albamu yake ya kwanza akiwa kama mmoja wa Def Jam, ilitoka mwaka wa 2006, ikiwa na jina la 'Hip Hop is Dead', ikiwa imeambatana na albamu nyingine ya mwaka wa 2008, iliyokwenda kwa jina la Untitled.
Albamu zake kwa ujumla.
1994: Illmatic
1996: It Was Written
1999: I Am…
1999: Nastradamus
2001: Stillmatic
2002: God's Son
2004: Street's Disciple
2006: Hip Hop Is Dead
2008: Untitled
Ikimbukwe kuwa hata nchini Tanzania kuliwahi kuzushwa kuwa Hip Hop inakufa
baada ya mdau mkubwa wa muziki kuwa na matatizo na wasanii wa Hip Hop wenye upeo mkubwa na kutaka kuwa katisha tamaa kwa kutumia akitumia msemo wa'Hip Hop is Dead'.Kufuatia hali hiyo ilibidi wasanii watoe nyimbo kali na kufanya jaamaa huyo abadilike tena na kuona aibu.
Wasanii walioonekana kubisha wakati huo ni Afande Sele na Tholothang.
PRO24 RADIO/TV
CLICK AND ENJOY GOOD MUSIC
MIXTAPES
ARTIST PROFILES
Blog Archive
LOVE LINKS
PRO-24 DJS OFFICIAL BLOG
PRO24 ENTERPRISES. Powered by Blogger.