Msanii nguli kwenye muziki wa Bongofleva Lucas Mkenda ‘Mr. Nice’ amesema baada ya kupokea maombi mengi ya mashabiki, ameamua kuanza kuwatendea haki wakazi wa Kanda ya Ziwa baada ya kumalizika kwa mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Akizungumza jijini Dar es Salaam Mr. Nice alisema kuwa amefurahi kuona mashabiki wake kutoka maeneo mbalimbali ndani na nje ya nchi, wanaendelea kumpokea vema tangu aliporejea kwenye medani ya muziki baada ya kuwa nje kwa miaka kadhaa.
Alisema hakutegemea kupata mapokezi makubwa namna hii wakati akiandaa albamu yake mpya ya ‘Tabia gani?’, aliyoikamilisha hivi karibuni, ambayo iko katika mahadhi ya mduara na ikionekana kufanya vema katika vituo vya radio na televisheni mbalimbali hapa nchini.
“Kaka nimepata mialiko mingi ya kufanya shoo katika mikoa kama, Shinyanga, Arusha, Mwanza, Kagera, Mbeya, Tanga pamoja na Morogoro, lakini mimi na wasimamizi wangu tumeamua kwenda Kanda ya Ziwa, lakini itakuwa baada ya kumalizika mwezi wa Ramadhani,” alisema Mr. Nice.
Aliongeza kuwa, pia amefurahi kuona wimbo wake mwingine uitwao ‘Mfalme’ aliowashirikisha wanamuziki kutoka Mexico na Hispania ukikubalika, hivyo katika kipindi cha mwezi wa Ramadhani atajifua na wacheza shoo wake tayari kuanza kazi.
PRO24 RADIO/TV
CLICK AND ENJOY GOOD MUSIC
MIXTAPES
ARTIST PROFILES
Blog Archive
LOVE LINKS
PRO-24 DJS OFFICIAL BLOG
PRO24 ENTERPRISES. Powered by Blogger.