Google PlusRSS FeedEmail

MZEE SMALL AANZA MAZOEZI YA VIUNGO

   
Mwigizaji wa muda mrefu wa filamu za Vichekesho nchini Saidi Mohamed 'Mzee Small', amesema kwa sasa hali yake kidogo inaanza kuwa na afadhari baada ya kuanza kuingia Gym kwaajili ya kuchukuwa mazoezi ya viungo vyake ambavyo vimepata kiarusi kutokana na ugonjwa wa presha ya kushuka. Akionyesha picha ya X -ray, ambayo inaonyesha mkono wake wa kushoto ukiwa umeachana kidogo kwa upande wa juu ya bega, pia mguu wakushoto nao ukiwa mzito anabuluza kwa kidogo. Aidha pia amesema kwa sasa maisha yake yanategemea sana, msaada wa watu wanaokuja kumuona. (Mzee Small na mkewe Fatma Saidi) Mzee Small alisema kwamba, ugonjwa huoaliupata June 17 aliporudi kutoka Mwanza akiwa na Bibi Chau, alipokuwa kwenye safari ya kukusanya wagonjwa wa ngozi Maarufu kama albino, ambao kwa sasa inafanywa na mzee Majuto. Aidha pia amewaomba wasanii kwamba wasimuogope kumshirikisha kwenye filamu zao kwakuwa wote wasanii na wanategemea  sanaa katika kuendesha maisha yao. Ila anadai kwamba wasanii wengi wanashindwa kumpa kazi kwa kuhofia ghalama kubwa kutokana na ukongwe wake katika sana hiyo. Alisema wala wasimuogope,kwani atakapopata nafuu wampe nafasi mbalimbali, kwakuwa hana ghalama kubwa kama wanavyodhani. Pia liongeza kwa kusema mkataba wake na Azam uliisha tangu mwaka jana, na sasa yupo huru.

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging