Google PlusRSS FeedEmail

RIHANNA ATOA CHOZI JUU YA KIFO CHA BIBI YAKE

Mwanamuziki wa R&B, Rihanna, ameeleza kuwa kifo cha bibi yake, Clara Brathwaite ‘Dolly’ ni pigo kubwa kwake na kwa familia yao. Akizungumza muda mfupi baada ya kuaga mwili wa bibi huyo katika chumba cha maiti cha Manthattan, ambapo alisema Dolly alikuwa zaidi ya bibi kwake. “Hakuwa bibi tu, bali alikuwa rafiki na mshauri wa mambo yangu mengi yakiwemo ya ujana nimekosa ushauri pamoja na sura yake nzuri niliyoipenda kuiona” alisema Rihanna
Alisema alizoea kumuona bibi yake akiwa nyumbani na wakati akihitaji ushauri alimfuata ili amtatutilie tatizo lake , pamoja na hayo katika ukurasa wake wa twitter,alisema “machozi makavu ,hata moyoni ni pakavu lakini nani atajali “maneno hayawezi kueleza uzuri wako ni wewe na wewe pekee hakuna mwingine
Kifo cha bibi huyo kimemuachia huzuni mwanamuziki huyo ambaye maisha yake yote ya ujana wake ameyatumia katika mikono ya bibi huyo

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging