Ndugu wawili Allain Mpela aliyekuwa Wenge BCBG na Geco Mpela aliyekuwa kwa Koffi Olomide kwa pamoja wametangaza kila mmoja kurudi kwenye game kivingine na kila mmoja akiwa na albamu yake.Afande Mpela yeye ndiye aliyeanza kutangaza nia kwa kuitangaza albamu yake ijayo inayoitwa Flèche empoisonnée (Mshale wa Sumu) na majuzi Geco Bouro Mpela ambaye alitamba kwa sauti nzuri na uchezaji wa madoido aliitangaza albamu yake itakayoitwa Bankoko.Ndugu hawa waliwahi kutoka na albamu ya pamoja iliyoitwa Mortal Combat, mi niliipenda ila huku nyumbani haikujulikana kwani haikuwahi kupewa Air Time kabisa.Kuna wakati Geco alitoka na single yake iliyoitwa intifada ambayo iliongozwa na kaka yake Allain Mpela ambayo kwa kiasi fulani ilikimbiza huko Congo na kwa mashabiki wa Congo Music kiujumla.
PRO24 RADIO/TV
CLICK AND ENJOY GOOD MUSIC
MIXTAPES
ARTIST PROFILES
Blog Archive
LOVE LINKS
PRO-24 DJS OFFICIAL BLOG
PRO24 ENTERPRISES. Powered by Blogger.








