MWIGIZAJI na mwandishi wa Muswada katika tasnia ya filamu Susan Lewis ‘Natasha’ amesema kuwa pamoja na kuwa ni mkongwe katika tasnia hiyo ya filamu sekta hiyo bado haitegemei kwa sababu hailipi jambo ambalo linamfanya ajikute akiwa makini na biashara yake ya ubunifu na ushonaji wa mavazi, kazi inayomlipa kuliko hata filamu. “Tasnia ya filamu hailipi kabisa, kuna wakati ambao unaona kabisa jinsi ukipoteza muda wako katika kuhangaika na jambo lisilo lipa wakati kwa wenzetu ni ajira rasmi, unatumia nguvu kubwa lakini linavyokuja suala la malipo au kuuza filamu husika unababaishwa na wanunuzi jambo linatengeneza mazingira ya wasanii kujikuta wakidhulumiana kutokana na mazingira yaliyopo,”anasema.
Natasha anasema kuwa anatumia muda mwingi katika kuchagua filamu za kushiriki ikiwa katika kuwaunga mkono wasanii wachanga lakini si katika kutengeneza fedha, huku akisema kuwa mara nyingi katika tasnia ya filamu kumekuwa na taarifa zisozo sahihi kutoka kwa baadhi ya wasanii ambao wamekuwa wakijinadi kuwa wanalipwa fedha nyingi kwa kushiriki filamu hizo.“Kuna wakati ambao baadhi ya wasanii wamekuwa wakidanya kama wanalipwa fedha kuanzia milioni kwenda mbele jambo hili si kweli, mfano filamu inawashiriki zaidi ya 20 kila msanii akilipwa milioni tu, ukichanganya na gharama za uandaaji filamu hiyo gharama zake zinaweza kufikia hata milioni 25, je ni filamu ngapi ambazo zinauzwa zaidi ya milioni 35? Hapo ndio utabaini ukweli,”anasema Natasha.