Google PlusRSS FeedEmail

KADINDA KUWAKILISHA NEW YORK


Mbunifu wa Tanzania Martin Kadinda ‘Single Button, anatarajia kuonyesha mavazi yake leo nchini Marekani katika onyesho la mavazi la New York Afrika Fashion Week na Music on The Caltwalk(MOC)

Akizungumza Dar es Salaam Mkurugenzi wa Kampuni ya One Touch Solutions, Petter Mwendapole alisema kuwa Martin atakuwa huko pamoja na wabunifu wengine saba kutoka sehemu mbalimbali za Afrika

“Martin ni mmoja wa wabunifu ambao wamechaguliwa kushiriki kwenye onyesho hilo litakaloambatana na utoaji tuzo kwa wasanii wa filamju na wanamuziki wengine wa Nigeria” alisema

Mbali na makoti maarufu ya Single Button , Martin ataonyesha pia nguo zake mpya ziitwazo vibunduki pamoja na Kivumbi Collection, ambazo kwa mara ya kwanza zilionyeshwa kwenye Dar Fashion Festival

Akizungumza nafasi ya kushiriki onesho hilo Kadinda alisema amefurahia kwa kuwa itampa nafasi ya kukutana na wabunifu wengine wakubwa duniani na kujifunza mambo mbalimbali katika sanaa

“Hii ni changamoto kubwa kwangu nitaitumia vizuri kuhakikisha naongeza ujuzi katika sekta ya ubunifu nashukuru kwa maandalizi ambayo One Touch wamefanya kwa ajili ya kunikutanisha na watu mbalimbali nchini Marekani watakaonipa maelezo juu ya kazi yangu “ alisema

Music On The Catwalk itafanyika Ukumbi wa Hellen Mills Event and Theater mjini New York

MOC ni onyesho kila kila mwaka, ambalo limebuniwa kwa ajili ya kukuza vipaji vya wasanii wa muziki pamoja na mavazi ambapo lengo kuu ni kutangaza kazi za wasanii wa Kiafrika

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging