Google PlusRSS FeedEmail

YAJUWE MAMBO YA LADY GAGA


Mwanadada asiyeishiwa vituko lskini skiwa na mafanikio makubwa katika muziki, Stefanni Joanne Angelina Germanotta maarufu kwa jina la kisanii kama ‘Lady Gaga’ ameendelea kuwa mwanamuziki mwenye mvuto pamoja na vituko mbalimbali.

Gaga ambaye alizaliwa Machi 28, 1986 ni muimbaji na mtunzi wa nyimbo wa kimarekani .alizaliwa na kukulia mjini New York alipata elimu yake katika shule ya Convent na baadaye kujiunga katika chuo kikuu cha New York katika idara ya sanaa na baadaye aliacha chuo na kuongeza bidii katika sanaaa ya muziki


Alianza kuimba ‘muziki wa rock’ maeneo ya Manhattan na mwisho wa mwaka 2007 alisaini mkataba na Streamline records,kwa kuajiliwa kama mtunzi wa nyimbo wa kampuni hiyo, uwezo wake wa kuimba uliweza kumshangaza msanii ambaye pia anarekodi Akoni ambaye alimsainisha katika lebo yake Kon Live Distribution

Lady Gaga alikuja kuwa maarufu kama msanii anayerekodi baada ya kuiachia albamu yake ya kwanza inayokwenda kwa jina la ‘The Fame’mwaka 2008ambayo ilikuwa imepikwa vizuri na kufanikiwa sana sokoni na kushikilia rekodi ya juu katika chati mbalimbali dunia nzima na kujumuisha vibao namba moja kimataifa vya juu ‘just Dance’ na ‘Poker Face’

Baada ya kuingia kwenye rebo hiyo alikuja na albamu ya ‘The fame Monster’ 2009 ambayo ilitoa vibao vilivyokuwa maarufu duniani vya ‘Bad Romance’’Telephone’ na Alejandro’na vikamruhusu kuingia katika ziara ya 18 ya Monster ambayo baadaye ilikuja kuwa moja kati ya ziara za kimuziki zilizokuwa na mafanikio makubwa katika historia ya muziki

Albamu yake mpya kabisa inayokwenda kwa jina la ‘Born This Way’ Judas na ‘The Edge of Glory’ mbali na masuala ya muziki Gaga pia ni mwanaharakati wa haki za binadamu, na haki za watu wa mapenzi ya jinsi moja huku akiwa mevutiwa na wasanii kama David Bowie, Michael Jackson, Madonna na Queen, Lady anajulikana sana kwa jinsi alivyokuwa na vipaji vingi tofautitofauti vinavyomfanya awe bora na kutoa mchango mkubwa sana katika sanaa ya muziki kama mwanamitindo kufanya vizuri jukwaani na kutoa video bora

Tayari ameshauza albamu milioni 23 na vibao vya kawaida milioni 64 dunia nzima vinavyomfanya kuwa kati ya wasanii wa muziki wenye mauzo makubwa kabisa katika historia ya muziki, mafanikio yake ni pamoja na kuingia mara nne katika kitabu cha rekodi ya dunia Guiness,tuzo tano za Grammy na tuzo 13 za MTV

Gaga ameshaingia mfurulizo katika chati za Billiboard kama msanii bora wa mwaka alishinda umaarufu wa kipekee mwaka 2010

Lady Gaga ni dada mwenye wadogo wawili Gaga anasisitiza kuwa ingawa anaonekana ametoka katika familia yenye uwezo yeye hajakulia kwenye familia ya kitajili kwa kusema “ wazazi wake wote wawili wametokea kwenye maisha ya chini kwa hiyo wametafuta kila kitu kwani mama yake amekuwa akifanya kazi kuanzia saa mbili asubuhi na kurudi saa mbili usiku muda wote anakuwa njee ya nyumbani akifanya kazi

Kuanzi akiwa na umri wa miaka 11 Gaga ambaye amekulia kwenye dhehebu la kikatoliki alijuunga na ’Convert of the Sacred Heart’ ambayo ni shule ya wasichana tupu iliyopo Manhattan’s katika jiji la New York

Alisema maisha yake ya shule yalikuwa ni ya kipekee sana yenye vituko na vimbanga vingi lakini kutokana kwamba hakuwa akiungwa mkono alijiona kama kioja mbele ya wenzake

Gaga alianza kupiga piano akiwa na miaka 4 akaendelea kuandika piano Ballard yake akiwa na miaka 13 na kuanza kupiga rasmi jukwaani akiwa na miaka 14

Gaga amekuwa pia ni mwanadada ambaye anasifika sana katika suala la mavazi ya ,mitindo tofauti inayovutia watu wengi ingawa mengi huwa yanakosolewa na watu mbalimbali kulingana na aina ya dhamira ya mavazi hayo huku yeye akiweka bayana kwamba sababu tofautitofauti nyingi zikiwemo katika harakati zake za kutetea haki za binadamu hasa haki za watu wa mapenzi ya jinsia zaidi ya moja

Huyo ndiye Gaga mwanamuzki mwenye vituko vinavyovuta hisia za mashabiki wengi wa muziki duniani

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging