Google PlusRSS FeedEmail
Showing posts with label ARTIST PROFILE. Show all posts
Showing posts with label ARTIST PROFILE. Show all posts

Said Ngamba au Mzee Small amezaliwa mwaka 1955 alikuwa msanii wa maigizo na vichekesho kutoka nchini Tanzania. Huenda akawa anaaminika zaidi kuwa ni mmoja wa wasanii wakongwe kwa nchi ya Tanzania, hasa katika fani ya uchekeshaji ambayo sasa inachezwa zaidi na vijana.

Mzee Small alizaliwa mwaka 1955 na kupata elimu yake ya msingi katika shule ya Mingumbi huko Kilwa mkoani Pwani. Mbali na kuwa mkongwe, pia Mzee Small kila unapozungumza naye huwa na kawaida ya kujitamba kuwa yeye ndiye msanii wa kwanza kabisa Tanzania Bara kuchekesha katika luninga.

Pamoja na kuwa yeye ndiyo mwanzilishi wa kuonyesha vichekesho kupitia luninga, lakini bado amesimama kufanya maigizo ingawaje alianza sanaa hiyo miaka 30 iliyopita na alipata kufundishwa na Bw.Said Seif ‘Unono’ (ambaye kwa sasa ni marehemu).

Mbali na kushiriki sanaa katika vikundi mbalimbali, pia Mzee Small amecheza sanaa katika vikundi vya mashirika kama vile Reli, NASACO na mengine mengi, ambayo kwa sasa hayajihusishi tena na shughuli hizo.

Mzee Small alianza kujulikana sana katika fani ya uchekeshaji hasa pale alipoibuka na mchezo unaojulikana kama 50, 50, 100, na ule wa Mjini Shule unaomwelezea mwanamke mmoja wa kijijini aliyeolewa mjini.

Mbali na kutamba na michezo hiyo, Mzee Small pia ni mcheshi na mwenye kupenda utani wakati wote, aliibuka na kichekesho kisemacho Nani Mwenye Haki.

Pia aliwahi kuibuka na kitu kingine kiitwacho “Nani Kama Shule" huku akiwa amewashirikisha wakina Majuto, Kingwendu nawachekeshaji wengine wanaotamba sasa nchini Tanzania.

Mzee Small alishawahi kumiliki kundi lake la sanaa linalojulikana kama Afro Dance ambalo alilisajili mwaka 1994 BASATA, na kupata usajili rasmi mwaka huohuo wa 1994.

Pamoja na kuwa na uzoefu wa kisanaa, lakini hakuwa na mpango wowote ule wa kujiunga na kundi jingine, ila anachoweza kufanya ni kurekodi na wasanii wengine atakapoitwa kwa makubaliano maalum. Mzee Small aliwahi kuzungumza hilo kwenye moja ya mahojiano aliyowahi kuyafanya kabla ya kufikwa na umauti.

Kutokana na vichekesho, Mzee Small huwa anatania kuwa sanaa ilimpa mke wa ndoa katika televisheni ambaye ni Bi Chau huku akianisha kuwa mkewe, Bi Fatuma huwa hana tatizo lolote na Bi Chau kwani anajua kinachoendelea kuwa ni kazi tu. Mzee Small ameacha watoto watano, watatu wa kiume na wawili wa kike

HALI YA UGONJWA

Wakati akiendelea na harakati za kisanaa, mwaka jana’ Mzee Small aliripotiwa kupatwa na ugonjwa wa kiharusi (stroke) alipokuwa kwenye shughuli za kisanaa Kanda Ziwa.Mzee Small amefikwa na umauti majira ya saa 4 za usiku Juni 7, mwaka huu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.

PROFILE: MZEE SMALL

Said Ngamba au Mzee Small amezaliwa mwaka 1955 alikuwa msanii wa maigizo na vichekesho kutoka nchini Tanzania. Huenda akawa anaaminika za... [Read More]


Jina Kamili : Joh Makini

Jina la Usanii : Joh Makini

Ulianza muziki lini? :  Alianza safari yake ya rasmi ya muziki wa Hip Hop mnamo mwaka 2003, huku akiamini hip hop ndio aina ya muziki anaouweza kuufanya kutokana na imani yake.

Nini unachokiamini katika imani ya Hip Hop? : Maisha yangu na imani yangu ni Hip Hop, sioni kitu kingine cha kufanya mbali na muziki, ingawa ndani ya muziki unafungua vitu vingine vya kuongezea kipato na ukipata fursa unatakiwa uvifanye kwa juhudi na ubunifu mkubwa ili viweze kutimiza malengo yako.

Kwa nini umeamua kufanya muziki wa Hip Hop: Nimeamua kufanya muziki huo kwa sababu anaamini muziki wa Hip Hop, na haoni muziki mwingine kuamini ambao anaweza kufanya kwani maisha yake anayoishi na imani yake aliyokuwa nayo yanamjenga kuendelea kuufanya muziki huo wa Hip Hop.

Kipindi cha mwaka huu nyimbo gani zilizoweza kufanya vizuri? : Kwa mwaka huu ameweza kutoa nyimbo mbili ambazo zimepokelewa vyema na mashabiki wake wa muziki wa kizazi kipya nchini, nyimbo hizo ambazo zinajulikana kwa jina la 'Bei ya Mkaa na Nikumbatie'.

Kwa nini bei ya Mkaa? : Bei ya mkaa ni nyimbo ambayo inazungumzia maisha ya kila siku, hivyo ni nyimbo inayogusa jamii moja kwa moja hiyo ndiyo sababu inayopelekea nyimbo hiyo kuendeleea kubaki kilele au kupokelewa vizuri na mashabiki wake.

Umefanikiwa kuingia katika tuzo Kilimanjaro? : Ni miongoni wa wasanii wa muziki wa Hip Hop aliyeingia katika kinyang'anyiro cha tuzo za Kilimanjaro ambapo baadhi ya wimbo zilizomuingiza katika tuzo hizo ikiwemo bei ya mkaa, pamoja na Nje ya Boxi iliyoimbwa na yeye pamoja na Nick wa Pili.


Mbali na muziki unafanya nini tena? : Mbali na muziki pia yeye ni mjasiriamali anayefanya biashara katika kampuni inayojulikana kwa jina la 'Weusi' huku akiwa ni miongoni mwa watu walioanzisha kampuni hiyo yenye lengo la kufanya kazi mbalimbali ikiwemo muziki wa Hip Hop.

Biashara gani unayojishughurisha nayo? : Joh Makini anajishughurisha na ubunifu wa tisheti, kofia, top za kike zenye nembo ya 'Nyeusi' ikiwa ni moja ya biashara ambayo imefunguliwa kutokana na kazi yao ya muziki.

Kwa nini umeamua kujiingiza katika ubunifu wa mavazi:  Ameamua kuwa mbunifu wa mavazi hao kama tisheti,na kofia kwa kuweka nembo ya Nyeusi ikiwa ni moja ya kazi zao na kukuuza muziki wao wa Hip Hop nchini kote na nje ya mipaka ya Tanzania.

Nini matarajio yako? : Anatarajia kuikuza biashara hiyo endapo mtaji wake ukiendelea kukua kwa kuanzisha biahsra pia ya viatu, na hata nguo za ndani za kiuume ili kuendeleea kutoa huduma za mavazi kwa mashabiki wake wa muziki .

Nguo unazobuni zinapatikana wapi? : Nguo hizo zinapatika katika maduka mbalimbali yalipo Kinondoni 'Bone to Shine' lililopo Kinondoni, ikiwa lengo lake ni kukuza biashara hiyo ya nguo huku ikienda sambamba na kazi yake ya muziki.

Mbali na biashara kitu gani kingine umewahi kufanya? : Mbali na biashara hiyo pia aliwahi kufanya kazi katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa Arusha (AICC)  kwa kipindi kifupi ingawa bado alikuwa akiendelee kufanya kazi yake ya muziki.





JOH MAKINI PROFILE

Jina Kamili : Joh Makini Jina la Usanii : Joh Makini Ulianza muziki lini? :  Alianza safari yake ya rasmi ya muziki wa Hip Ho... [Read More]


Jina Kamili :   Ibrahim Mussa

Jina la kisanii :  Roma Mkatoliki

Msanii wa miondoko : Roma ni msanii mkali wa Hip Hop Tanzania, ambaye tangu aanze kazi yake ya muziki amekuwa akiimba miondoko hiyo ya Hip Hop.

Alianza safari ya muziki lini ? : Safari yake ya muziki alianza mnamo mwaka 2006 akiwa mkoani Tanga, ingawa inadaiwa kuwa alitoroka shule asubuhi ili aweze kuonana na mtangazaji maarufu B. Twelve ambaye alienda mkoani hapo kwa ajili ya shoo.

Lini aliingia studio ? :  Mwaka 2007 aliweza kurekodi nyimbo yake ambayo aliipa jina la 'Salute' ambayo alifanya studio ya Gomba Record.

Sigle yake ya kwanza alitoa lini ?:  Mnamo mwaka 2008 aliweza kufanikiwa kurekodi nyimbo inayojulikana kwa jina la 'Tanzania' ambayo ndio miongoni mwa nyimbo ambayo imemtambulisha kwenye gemu la muziki nchini.

 Aliweza kuingia studio :  2007 niliweza kurecod ngoma ya kwanza iliyokuwa inajulikana kwa jina la SALUTE kwa producer abbuy .

Alifika Dar Lini ?: Mwaka 2008 ndio mwaka ambao nimeweza kufika dar rasmi kuishi na kuweza kurekodi TANZANIA .

Mbali na muziki anafanya nini? :  Mbali na kuwa msanii wa Hip Hop pia ni mchezaji mpira wa kikapu ambapo ameanza kucheza akiwa mdogo mtaani kwao ambapo alikuwa na timu ya mpira wa kikapu huku akiwa na ndoto ya kuwa mchezaji maarufu igawa ndoto hizo zimezimwa na muziki.

Alianza kucheza mpira wa kikapu lini?:  Roma alianza kucheza mchezo huo akiwa mdogo, huku akichezea timu yake ya mtaani akiwa anacheza namba 1,na 2 ingawa mwili wake unaonekana anaweza kucheza namba 5 kama 'big'.

Awa kocha:  Baada ya kuacha kucheza mchezo huo, ameweza kuendeleleza kipaji chake cha mchezo huo wa mpira wa kikapu ambapo ameweza kuwa kocha wa timu yake ya mtaani.

Sababu zilizosababisha awe kocha wa mpira wa kikapu : Kwa sasababu anapenda kuendelea kucheza mchezo huo wa mpira wa kikapu aliamua kujiunga kuwa kocha ili aweze kuendeleza kipaji chake.

Amejikita na masuala ya ujasiliamari : Mbali na kucheza mchezo huo pia ni mjasiriamali ambaye ameanza kufanya biashara mara baada ya kuanza kufanya muziki wake wa miondoko ya Hip Hop.

Mwanafunzi wa chuo:  Pamoja na hayo yeye ni mwanafunzi wa ngazi ya Stashahada  ambapo anampango wa kuendelea kujiendeleza na elimu ya chuo huku akidai kuwa elimu ni moja ya jambo ambalo anaamini ataliendeleza.

Ameshapokea tuzo ngapi?: Ameshawahi kupokea tuzo mbili za muziki wa Kilimanjaro, ameshapokea tuzo ya msanii bora wa Hip Hop kwa kupitia wimbo wake wa Mathematics, na wimbo bora wa Hip Hop. 

Kitu ambacho hawezi kukisahau?:  MWAKA 2006 akiwa tanga amewahi kutoroka shule asubuhi akamfwata B.TWELVE aliyekuja tanga nadhani kwenye show ya park lane, alifanikiwa kukutana naye kwenye gari na kumkabidhi cd zenye nyimbo mbili ambazo alimuomba azipige lakini hazikufanikiwa.




ROMA PROFILE

Jina Kamili :   Ibrahim Mussa Jina la kisanii :  Roma Mkatoliki Msanii wa miondoko : Roma ni msanii mkali wa Hip Hop Tanzania,... [Read More]



Tabu Ley: Mshumaa uliozimika kimyakimya *Aacha watoto 68 akiwa na miaka 76

JINA KAMILI : Pascal-Emmanuel Sinamoyi Tabu, ni mwanamuziki nguli wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC).

JINA LA KIMUZIKI : Maarufu kwa jina la Tabu Ley Rochereau.

MWANAMUZIKI WA AINA GANI? Alikuwa ni mwanamuziki wa miondoko ya Afrika ya aina ya Rhumba

AMEFARIKI : Amefariki Dunia Novemba 30, mwaka huu

AMEZALIWA : Tabu Ley alizaliwa Novemba 13, kati ya mwaka 1937 katika mji wa Bagata kwenye nchi iliyokuwa ikijulikana kama Congo ya Ubelgiji (Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo).

ANAWATOTO WANGAPI? Anawatoto 68 ambao amezaa na wanawake tofautitofauti.

SAFARI YAKE YA MUZIKI : Alikuwa kiongozi wa bendi ya muziki wa dansi iitwayo Orchestre Afrisa International na alikuwa mmoja wa waimbaji wa Afrika wenye mvuto na mtunzi mahiri.

ALIFANYA VITU GANI KUBORESHA MUZIKI WAKE : Akiwa pamoja na mpiga gita mashuhuri Dkt. Nico Kasanda, Tabu Ley alikuwa mwasisi wa mtindo wa soukous (Rumba ya Afrika) na muziki wake aliufanya kuwa wa kimataifa kwa kutia vionjo vya muziki wa asili wa Congo na rhumba la Cuba, Caribbean na Latin America.

MTU MASHUHURI WA CONGO : Tabu Ley au ukipenda Rochereau, anaelezewa kama 'mtu mashuhuri' wa Congo ambaye, pamoja na Rais Mobutu Sese seko, waliweka historia ya Afrika katika karne ya 20."

JINA ALILOPEWA KUTOKANA NA KAZI YAKE : Kutokana na umahiri wake katika muziki wa rhumba, Tabu Ley aliwahi kupewa jina la "Elvis wa Afrika" na gazeti la 'Times' la Los Angeles nchini Marekani.

MBALI NA MUZIKI ALIKUWA MWANASIASA : Baada ya kuangushwa utawala wa Mobutu, Tabu Ley pia aliingia katika siasa.

JUMLA YA NYIMBO ALIZOTUNGA : Wakati wa enzi zake, Tabu Ley aliweza kutunga nyimbo mpaka 3,000 na kutoa albamu 250.

ALIANZA MUZIKI LINI?: Tabu Ley au Rochereau, alianza kazi ya muziki mwaka 1956 wakati alipoimba pamoja na Joseph Kabasele Yampanya 'Pepe Kalle' akiwa na bendi yake ya African Jazz.

Baada ya kumaliza kidato cha sita, Tabu Ley aliamua kuwa mwanamuziki wakati wote. Tabu Ley alitoa wimbo uitwao 'Cha Cha' kusherehekea uhuru wa Congo kutoka Ubelgiji mwaka 1960.

ALIFANYA MUZIKI NA WASANII GANI? Wimbo huu wa 'Cha Cha' ulitungwa na Pepe Kalle, ambapo ulimpaisha Tabu Ley na kupata umaarufu kwa haraka sana. Tabu Ley alibaki na bendi ya African Jazz mpaka mwaka 1963 wakati yeye na Dkt. Nico Kasanda walipounda bendi yao, African Fiesta.

ALIFUNGUA BENDI: Miaka miwili baadaye, Tabu Ley na Dkt. Nico walisambaratika na Tabu Ley akaunda bendi yake ambayo ilikuwa ikijulikana kama African Fiesta National, na pia ilijulikana kama African Fiesta Flash.

Bendi ya African Fiesta National ilikuwa moja ya bendi zenye mafanikio makubwa katika historia ya muziki wa Afrika, ikirekodi nyimbo kali kama 'Afrika Mokili Mobimba'.

WIMBO GANI ULIOVUNJA REKODI YA MAUZO ? Wimbo Wa 'Afrika Mokili Mobimba' ilivunja rekodi ya mauzo kwa kuuza nakala milioni moja mwaka 1970.

Wakati huo, Papa Wemba na Sam Mangwana walikuwa miongoni mwa wanamuziki waliotakatisha kundi la African Fiesta National.

JINA GANI LA JUKWAA ALILOCHUKUA? Tabu Ley alichukua jina la jukwaa la 'Rochereau' kutoka kwa Generali wa Jeshi la Ufaransa, Pierre Denfert-Rochereau, ambaye alisoma naye shule moja na kulipenda jina lake.

SAFARI YA BENDI : Mwaka 1970, Tabu Ley aliunda bendi ya Orchestre Afrisa International, Afrisa ikiwa ni mchanganyiko kati ya jina Afrika na Isa, alama ya muziki wake.

Akiwa pamoja na Franco Luambo Makiadi wa TPOK Jazz, Afrisa ikawa moja ya bendi kubwa barani Afrika. Walirekodi vibao kama 'Sorozo', 'Kaful Mayay', 'Aon Aon', na 'Mose Konzo'.

ALIVUMBUA VIPAJI VIPYA : Katikati ya miaka ya 1980, Tabu Ley aliweza kugundua kipaji cha mwanadada mwimbaji na mcheza shoo, M'bilia Bel, ambaye alichangia sana kuipaisha bendi ya Orchestre Afrisa International.

M'bilia Bel alikuwa mwimbaji mwanamke wa kwanza wa muziki wa soukous, ambaye alijipatia umaarufu Afrika yote.

MAISHA YA MAPENZI : Tabu Ley na M'bilia Bel baadaye walifunga ndoa na kupata mtoto mmoja. Mwaka 1988 Tabu Ley alimuibua mwanamuziki mwingine wa kike ajulikanaye kama Faya Tess.

Kuona Faya Tess ananyanyuka kwa kasi,  M'bilia Bel aliamua kuondoka katika bendi hiyo na kuendelea kufanya vizuri katika kazi za muziki akiwa kivyake.

Baada ya M'bilia Bel kuondoka, mvuto wa bendi ya Afrisa pamoja na ule wa wapinzani wao TPOK Jazz uliendelea kufifia kutokana na mashabiki kugeukea mtindo mpya wa muziki wa soukous wenye kasi zaidi.

Baada ya utawala wa Rais Mobutu Sese Seko kuanzishwa katika Congo, Rochereau akachukua jina la 'Tabu Ley' kama sehemu ya kampeni ya Mobutu kuwafanya wananchi wa Zaire kuwa na majina ya asili.

SABABU ZILIZOMFANYA ATOROKE: Hata hivyo, mwaka 1988 Tabu Ley alitoroka na kwenda kuishi uhamishoni nchini Ufaransa.

Mwaka 1985, Serikali ya Kenya ilipiga marufuku muziki wa kigeni kuchezwa kwenye Redio ya Taifa.

Baada ya Tabu Ley kutunga wimbo 'Twende Nairobi', aliouimbwa na M'bilia Bel, kumsifu Rais wa Kenya wakati huo, Daniel Arap Moi katazo hilo mara moja likaondolewa.

Mapema 1990 Tabu Ley aliishi kwa muda mfupi Kusini ya California nchini Marekani. Alianza kutengeneza muziki wake kuwa wa kimataifa zaidi na kuingiza lugha ya Kingereza na kuongeza staili za kucheza kuwa za kimataifa zaidi kama vile Samba.

Rochereau aliona kupata mafanikia kwa kutoa albamu kama Muzina, Exil Ley, Africa worldwide na Babeti soukous.

Utawala wa Mobutu ulipiga marufuku albamu yake ya mwaka 1990 iitwayo 'Trop, C'est Trop' ambayo aliiona kama inamchafua. Mwaka 1996, Tabu Ley alishiriki katika albamu iitwayo Gombo Salsa iliyotolewa na bendi ya Africando.

Wimbo wa 'Paquita' kutoka albamu ya Gombo ni moja ya wimbo uliowahi kurekodiwa mwishoni mwa miaka ya 1960 na bendi ya African Fiesta.

Wakati Rais Mobutu Sese Seko alipoondolewa madarakani mwaka 1997, Tabu Ley alirudi Kinshasa na kupewa Uwaziri katika serikali mpya ya Rais Laurent Kabila.

Kutokana na kifo cha Laurent Kabila, Tabu Ley kisha alijiunga na Bunge teule la mpito lililoundwa na Joseph Kabila, mpaka lilipovunjwa baada ya kuundwa kwa taasisi za mpito.

CHEO ALICHOPATA : Novemba 2005, Tabu Ley aliteuliwa kuwa Kaimu Gavana Kinshasa, nafasi aliyopewa kutokana na chama chake cha Congolese Rally for Democracy, kutokana na makubaliano ya amani 2002.

AMESHWAHI KUWA WAZIRI : Tabu Ley aliyewahi pia kuwa Waziri wa Utamaduni, inasemekana amezaa watoto 68 na wanawake tofauti tofauti, akiwemo rapa mashuhuri wa Ufaransa, Youssoupha.

Rochereau amekufa akiwa na umri wa miaka 76 katika Hospitali ya Mtakatifu Luc mjini Brussels, Ubelgiji ambako alikuwa akipata matibabu ya ugonjwa wa kiharusi uliomkumba mwaka 2008.

TABU LEY ROCHEREAU : PROFILE

Tabu Ley: Mshumaa uliozimika kimyakimya *Aacha watoto 68 akiwa na miaka 76 JINA KAMILI : Pascal-Emmanuel Sinamoyi Tabu, ni mwanamuzik... [Read More]






Jina Kamili : Kala Masoud

Jina la Kisanii : Kala Pina

Msanii wa miondoko : Kala Pina ni msanii wa miondoko ya Hip Hop nchini ambapo yupo katika kundi la Kikosi cha mizinga.

Mbali na muziki : Msanii wa Hip Hop nchini Kala Pina pia anajishughurisha na masuala ya Siasa na kilimo ambapo alizama kwenye siasa huku akiamini kuwa Tanzania ni nchi ya demokrasia.

Mchakato wa siasa alianza lini ? Alijiingiza katika masuala ya siasa mnamo mwaka 1995 ambapo alijiiunga na chama cha Wananchi Cuf huku akiwa mwanachama hai kwa kuugawa muda wake kuhudhuria vikao mbalimbali vya kichama.

Hali ya uongozi ndani ya chama: Mnamo mwaka 2011 aliweza kupata nyadhifa mbalimbali za uongozi ndani ya chama hicho ambapo aliweza kupata nafasi ya kuwa Naibu Katibu Mkuu Umoja wa Vijana CUF.

Mchango ndani ya chama : Anaamini ndani ya chama hicho anamchango mkubwa ikiwemo wa kuhamasisha vijana wengi kujiunga ndani ya chama hicho ili kuleta changamoto kwa vijana hususani suala la kimaendeleo.

Mkulima : Mbali na kujiunga na masuala ya chama pia anajishughurisha na shughuri za kilimo cha umwagiliaji huku akiamini kuwa kuongeza kipato kwenye upande huo.

Maeneo : Anajishughurisha na kilimo hicho maeneo ya Rufiji mkoa wa Pwani, ambapo analima kilimo cha umwagiliaji mazao ya nafaka kwa ajili ya biashara.

Elimu yake : Amejikita katika suala hilo kutokana na elimu aliyoipata alipokuwa shule kwani alisoma masomo ya kilimo.

KALA PIINA PROFILE

Jina Kamili : Kala Masoud Jina la Kisanii : Kala Pina Msanii wa miondoko : Kala Pina ni msanii wa miondoko ya Hip Hop nchini... [Read More]

Jina kamili :  Taikuni Ally

Jina la Kisanii : Mchizi Moxie  hilo ndio jina linalomtambulisha kwenye sanaa ya muziki  wa hip hop , ni miongoni mwa vijana ambaye alijiunga na fani ya muziki wa kizazi kwa ajili ya kuendeleza kipaji chake pamoja na kuinua kipaji chake.

Alianza safari yake ya muziki lini ?: Mchizi Mox alianza safari yake ya muziki akiwa masomoni kwa kujiunga na bendi ya shule, kuimba pamoja wanafunzi wenzake, huku akiwa na ndoto ya msanii mkubwa nchini.
Mchizi Mox aliamini juhudi ndizo zitakazomfanikisha mafanikio yake, kutokana na hilo aliamua zaidi kujikita katika mambo ya sanaa hata kupiga ngoma mbalimbali alipokuwa masomoni.

Ushirikiano alioupata : Akielezea historia yake kwa ufupi msanii huyo aliweka wazi kuwa, aliamua kujiunga na na mambo ya sanaa ya muziki wa kizazi kipya huku akipata ushirikiano kutoka kwa wazazi wake.

Kabla ya kundi la Wateule alitokea wapi? : Kabla ya kuunda kundi la Wateule, Moxie aliweza kufanikiwa kutoa single iliyojulikana kwa jina la 'Watoto wa mitaani' nyimbo iliyobeba ujumbe na kuelimisha jamii juu ya kudhibiti na kupunguza watoto wa mitaani. Aiweza kufanikiwa kurekodi nyimbo hiyo kwa msaada wa mama yake ambaye alimpa ushirikiano wa kwenda studio kurekodi ikiwemo kumlipia gharama zote za studio.

Safari ya muziki ilianza wapi ? : Baada ya muda Moxie aliweza kunga'ra akiwa na wenzake Jafarray pamoja na Jaymoe kwa kushinda katika mashindano ya kuibua vipaji vya muziki ambapo waliteuliwa kuwa ni kundi bora la Hip Hop.

Jina la Wateule lilianza kipindi gani ? : Hapo ndipo kundi la 'Wateule' lilipoanza katika studio ya bongo records, baada ya kufika katika studio hizo washindi hao kwa ajili ya kurekodi nyimbo ikiwa zawadi ya ushindi huo ndipo jina la wateule lilipozaliwa.

Safari ya muziki alianza lini ?: Msanii huyo alianza safari yake ya muziki mnamo 2000, pamoja na kuunda kundi hilo la wateule na kufanikiwa kutoa 'single' iliyokuwa inawatambulisha katika jamii.

Undani wa kundi la Wateule : Baada ya muda kidogo kundi hilo lilivunjika ambapo kila mmoja alianza kufanya kazi kwa mtindo wa pekee yake, hivyo Moxie alibaki kwa muda bila ya kutoa nyimbo yoyote kwenye jamii hali hiyo ilimpa changamoto kwa mashabiki wake.

Baada ya kuvunjika kwa kundi : Baada ya kimya cha muda mrefu Moxie aliendeleza kundi hilo la Wateule kwa kutoa nyimbo iliyojulikana kwa jina la 'Watu kibao' miaka 2001 ambapo nyimbo hiyo iliibua hisia kwa mashabiki walioisahau kundi la wateule.Aliweza kufanya vyema katika mambo ya muziki huku ndoto zake ni kuendelea kuwa msanii mkubwa, aliweza kufanikisha malengo yake kwa kutoa single nyingine ambayo ilimtambulisha Mox katika suala zima la muziki.

Nyimbo iliyomtambulisha kwenye gemu : Nyimbo ya 'Mambo vipi' ilikuwa ni jibu kwa Moxie ambapo aliweza kuibua na kuteka hisia za mashabiki wake huku akiendelea kuongeza mashabiki lukuki kutokana na ujumbe pamoja na aina ya uimbaji wa nyimbo hiyo huku sauti yake ikiendelea kuwa mvuto ndani ya nyimbo.

Mapokeo ya wimbo Mambo vipi : Mambo vipi, ilimuongezea mashabiki lukuki huku, pamoja na kuongeza imani kwa wasanii wenzake huku baadhi yao wakiwa na kiu ya kushirikiana nao katika kazi ya muziki.

Anachokipenda: Moxie anajivunia mvuto wa sauti yake ambayo imemfanya kumuongezea kufanya kazi na wasanii wengi huku baadhi yao wakiamini kuwa ubora wa sauti yake ndiyo inaweza kuboresha nyimbo anazoshirikishwa.

Anapenda nini kwenye kazi: Moxie  ambaye amefanya kazi za kushirikishwa na wasanii wengi hapo mwanzo, sasa ameweka bayana msimamo wake wa kutofanya kazi za kushirikishwa kwani anaona hazina faida kwake.Moxie baada ya ukimya wa muda mrefu sasa anajipanga kurudi tena kwenye gemu kwa kuachia albamu yake ya pili ambayo ataipa jina la 'Goli la pili na mwisho wa mchezo' ikiwa ndio albamu yake ya mwisho huku albamu yake ya kwanza aliipa jina la 'Goli la kwanza'

Msanii huyo aliweka wazi kuwa hana mpango wa kuendelea kutoa albamu kwani albamu hizo hazilipi ila anayoitoa ni ya mwisho na kuendelea kubaki kutoa single.Moxie ameachia nyimbo inayokwenda kwa jina la Piga makofi yenye mahadhi ya regga.

MCHIZI MOXIE PROFILE

Jina kamili :  Taikuni Ally Jina la Kisanii : Mchizi Moxie  hilo ndio jina linalomtambulisha kwenye sanaa ya muziki  wa hip hop , ni m... [Read More]


Jina kamili : Farid Kubanga

Jina la usanii : Fid Q.

Amezaliwa : 13 Agosti katika hospitali ya Bungando iliyopo jijini Mwanza .

Alianza muziki lini :  Fid Q alianza shughuli za muziki mnamo miaka ya 1990. Alitoa kibao chake cha kwanza mwaka 2000 kiitwacho 'Huyu na Yule' ambacho hicho aliimba na msanii Mr Paul. Kibao hiki kilimpa heshima kubwa, kibao hicho kilirekodiwa katika studio za MJ records chini ya usimamizi wake Master Jay mwenyewe.

Single ya pili aliitoa lini : Kibao chake cha pili kutoka kiliitwa 'Binti Malkia'. ambacho alimshirikisha Noorelly. Ilivyofika mnamo mwaka wa 2004 Fid Q alivunja ukimya wake kwa kibao chake mahili kilichokwenda kwa jina la "Fid Q.com", na kibao hicho alikifanya katika studi ya Baucha Records baada ya kuhama kwa MJ.

Kibao hicho kiliirudisha ile hiphop ya Tanzania katika ramani yake halisi na inasemekana hivyo kwasababu kipindi hicho ni kile ambacho wasaanii wengi wa muziki wa kufokafoka walikuwa wamejiingiza katika masuala ya uimbaji kwasababu kulikuwa na uvumi wa kwamba hip hop haikubaliki kwa watu wa Tanzania.

Ilipofika mwezi wa Januri ya 26 katika mwaka wa 2008, Fid Q alipakua kibao kiitwacho "Ni Hayo Tu" alichomshirikisha Prof. J na Langa.

Jumla ya albamu : Fid Q ana albamu mbili kwenye soko la muziki. Albamu ya kwanza inaitwa inayoitwa "Vina Mwanzo Kati na Mwisho".[1] Mwishoni mwa mwaka 2009 alitoa albamu ya pili "PROPAGANDA", ambayo imepokelewa vizuri sana Tanzania na nchi nyingine za Afrika Mashariki.

 Mashabiki wa Hip Hop wanaichukulia PROPAGANDA kama ni albamu bora kabisa, yaani 'classic'. Hivi karibuni anategemea kutoa albamu yake ya tatu itakayokwenda kwa jina la "KitaaOLOJIA".

HAPPY BIRTHDAY FID Q

Jina kamili : Farid Kubanga Jina la usanii : Fid Q. Amezaliwa : 13 Agosti katika hospitali ya Bungando iliyopo jijini Mwanza . Alia... [Read More]



Jina kamili :  Mohamedi Mwikongi

Jina la Usanii : Frank ni  mmoja wa waigizaji wakongwe  ndani ya tasnia ya filamu nchini

Umezaliwa wapi ? Frank amezaliwa  jijini Dar es salaam mwaka 1979 katka hospitali ya ocean road.

Amepata elimu yake :  Alipoanza kukua alihamia Mkoani Iringa ambako alipata elimu ya awali katika  shule ya msingi Wiloseli kabla ya kuhamia shule ya msingi Mapambano jiji Dar es salaam ambako alimaliza elimu yake ya msingi.

Baada ya hapo alijiunga ma shule ya sekondari ya Highlands ilyopo wilayani iringa ambako alisoma na kuweza kuhitimu masomo yake ya O’level. Baadaye alijiunga na shuke ya sekondari Jitegemee kwa elimu ya kidato cha tano na sita na mwishowe kumaliza safari ya elimu katika Chuo cha kodi (ITA) cha TRA jijini Dar es salaam


Lini ulianza kuigiza ? Frank alianza Rasmi kuigiza mnamo mwaka 1999 chini ya kikundi cha Fukuto arts group kilichokuwa kikirusha maigizo yake kwenye kituo cha ITV kabla ya kujiunga na kikundi cha Kaole sanaa group ambako aliweza kupata umaarufu mkubwa na kujenga jina lake la frank kwenye igizo la Tufani.

Safari yake ya kuigiza ilikuaje ? : Aliweza kuigiza katika  kuigiza kwenye filamu mbalimbali na baadhi ya filamu zilizompa umaaarufu ni pamoja na Dangerous Desire, Sikitiko langu, behind the scenes na nyingine nyingi

Akiwa katika mapumziko Mohamedi anapenda zaidi kufanya mazoezi na kumpumzika


PROFILE : MOHAMEDI MWIKONGI (FRANK)

Jina kamili :  Mohamedi Mwikongi Jina la Usanii : Frank ni  mmoja wa waigizaji wakongwe  ndani ya tasnia ya filamu nchini Umezaliwa ... [Read More]



Jina Kamili : FATMA binti Baraka

Jina la kisanii : Maarufu kwa jina la Bi Kidude, ni miongoni mwa wasanii wanawake wachache ambao ni magwiji wa muziki wa taarabu nchini,

Amezaliwa :  ni mzaliwa wa Zanzibar lakini asili ya kabila lake ni Mmanyema kutoka Mkoa wa Kigoma, magharibi mwa nchi.

Umri : Miaka 113

Ana watoto wangapi ? : Hajabahatika kupata mtoto ingawa aliwahi kuolewa mara mbili

Muziki alianza lini ? : Mkongwe huyo wa muziki  amekuwa muimbaji tangu miaka ya 1920 akiwa ni mfuasi wa Sitti Bin Saad mmojawapo wa waimbaji wa mwanzo kabisa wa taarabu visiwani Zanzibar.

Kazi ya muziki : Bi. Kidude aliweza kuteka soko la muziki hususani wa mwambao kwa kutunga mashahiri yaliyobeba ujumbe wa mahaba pamoja na mafumbo kwa lugha ya kiswahili yenye lengo la kufikisha ujumbe wake kwa mashabiki wake

Nyimbo zilizofanya vizuri : Nyimbo zake zilizoweza kufanya vizuri ikiwemo  Yalait, Muhogo wa Jang’ombe,  Kijiti, Arebaba na  Machozi ya huba

Asili ya jina lake : Kwa mujibu wa taarifa ya vyombo  tofauti vya habari Bi. Kidude alielezea asili la jina lake kuwa alipewa na mjomba wake wakati alipozaliwa kwa sababu alikuwa na umbile dogo.


Safari yake ya muziki : Akiwa na umri wa miaka 13  hakuwa na jinsi bali kukimbilia Tanzania bara(Tanganyika enzi hizo) ili kuepuka kuozeshwa kwa nguvu. Akiwa Tanzania bara alizunguka kila kona ya nchi akiwa muimbaji katika makundi mbalimbali ya muziki wa taarabu likiwemo lile maarufu la Egyptian Musical Taarab. Baadaye alihamia nchini Misri kwa kifupi kabla hajarejea kisiwani Zanzibar mahali ambapo umauti wake ulipomkuta.

Tuzo za muziki : Amewahi kupokea tuzo mbalimbali  mwaka 2005 , nchini Uingereza,ambapo alipokea tuzo yenye heshima kutoka World Music Expo (WOMEX) kwa mchango wake katika muziki na utamaduni wa Zanzibar. Katika kinyang’anyiro hicho aliwashinda wanamuziki mahiri kama Peter Gabriel, Miriam Makeba na wengineo.

Aliyeibua kipaji chake : Mtu wa kwanza kuthamini kazi za kumtafuta hadi kufika alipo alikuwa Rais mstaafu wa Tanzania wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi.

Ziara ambazo amewahi kufanya : Aliwahi  kufanya ziara nchini Uingereza kwa Malkia Elizabeth II , ambao alipewa zawadi ya  kidani cha dhahabu ikiwa ni moja ya kuthamani kazi yake. ziara ya pili ya muimbaji huyo ilikuwa nchini Ujerumani  ambapo aliweza kusimama kwenye majukwaa na kutumbuiza.

Ameishi : Kutokana na umahili wa uimbaji wake pamoja na kuwa na mashahiri yenye ubunifu huku akikitangaza kiswahili aliweza kuishi nchini Ajipshini (Egyptian) kwa miaka tisa kutokana na kazi hiyo ya muziki

Kazi nje ya muziki : Ameweza kuwa mmoja wa wasanii waliohudhuria uzinduzi wa kampeni ya Malaria iliyokwenda kwa jina la 'Zinduka' kwa kuhudhuria kampeni hiyo aliweza kukonga nyoyo ya Rais Kikwete

Sifa ya Bi. Kidude : Kuimba kwa kutumia  kichwa na dhati ya moyo wake kwenye kuimba kwani  kubana au kuibadili sauti wakati wa kuimba si sahihi, inamtoa mwimbaji kwenye uhalisia wake.


Uvutaji wa Sigara : Sifa yake nyingine kuwa alikuwa na uwezo wa kuvuta sigara ambapo kwa siku alikuwa anauwezo wa kuvuta pakiti moja kwa siku tatu huku sauti yake ikiwa bado ipo imara

Hali ya ugonjwa wake : Bi. Kidude alianza kuumwa mwishoni mwa mwaka jana akiwa akisumbuliwa na maradhi ya sukari, ambayo ni maradhi yake ya muda mrefu ila yalizidi baada ya kukiuka taratibu za vyakula

PROFILE : BI. KIDUDE

Jina Kamili : FATMA binti Baraka Jina la kisanii : Maarufu kwa jina la Bi Kidude, ni miongoni mwa wasanii wanawake wachache ambao ni ... [Read More]



Jina kamili : Willow Camile Smith

Kazi anayofanya 

Yeye ni muimbaji kutoka nchini Marekani

Mwaka aliozaliwa:

Amezaliwa oktoba 31 mwaka 2000

Ni mtoto wa nani ?

Ni mtoto wa mkongwe wa muziki na filamu Will Smith na Jada Pinkett Smith ambaye pia ni kama mume wake

Lini alianza kuonekana katika ulimwengu wa filamu ? :

Willow alianza kuonekana katika ulimwengu wa filamu mwaka 2007 alipoigiza 'Im Legend' na baadaye alionekana katika 'Kit Kitredge'


Tuzo alizopata?

Filamu hizo mbili zilimfanya apate tuzo ya kuwa msanii bora chipukizi kutokana na uwezo mkubwa aliouonyesha huku akiwa na umri mdogo

Lini alianza muziki?

Mwaka 2010 ndipo alijikita katika tasnia ya muziki baada ya kutoa 'single' yake ya kwanza 'Whip My Hair' na 21 Girl Century

 Nani aliyevutiwa na kazi yake hiyo ?

Nyimbo hizo mbili zilimvutioa mtayarishaji mkongwe na muimbaji wa Hip Pop Jay Z ambapo alimpa mkataba katika studio ya Nation Roc

katika familia yao wako wangapi?

Willow anandugu zake wawili Trey Smith ambaye amechangia baba na Jade Smith

Mbali na muziki:

Willow na ndugu zake ni mabarozi vijana katika kwa ajili ya maradi wa Zambia ambayo unatoa msaada kwa watoto yatima wazazi wao walifariki kutokana na UKIMWI kwa kushirikiana na Hasbro

Wanamchakato gani ?

Kwa sasa Willow na ndugu yake wapo katika mchakato wa kutoa albamu mpya ya pamoja baada ya mama yao Jada kuthibitisha hilo

Wasanii wengi wa nchi zilizoendelea wamekuwa wakihakikisha vizazi vyao vinafuata mfano wa shughuli zao ambazo baadaye wanakuwa nyota na kutamba anga mbalimbali

Hii tumewahi kuwashuhudia wakali mbalimbali ambao watoto wao wakianza kupata akili huanza kuwafundisha fani mbalimbali iwe kwa upande wa wanamuziki, waigizaji au hata kwa wacheza mpira huakikisha kizazi chao kinafuata nyayo hizo katika siku za usoni



WILLOW SMITH - PROFILE

Jina kamili : Willow Camile Smith Kazi anayofanya  Yeye ni muimbaji kutoka nchini Marekani Mwaka aliozaliwa: Amezaliwa oktoba ... [Read More]



Jina Kamili : Nika Tanya Maraj

Jina analotumia kimuziki : Nick Minaj

Mahali alipozaliwa : 

Alizaliwa Saint James Trinidad na alipokuwa na umri wa miaka 5 alihamia New York City

Yeye ni nani : 

Ni rapa, muimbaji, mtunzi wa nyimbo na muigizaji wa televisheni kutoka nchini Marekani

Kazi ya muziki alianza lini ? :

Kipaji chake kilionekana kati ya  mwaka 2007 na 2009 wakati alipotoa nyimbo zake zilizowavutia Young Money Entertainment ambao waliingia naye mkataba

Aliyemvutia kuingia kwenye sanaa hiyo ya uimbaji:

Minaj alikiri kabla ya kuimba alivutiwa na Lisa Lopes "Left Eye", Lil Wayne, Lauryn Hill, Jadakiss, Natasha Bedingfield, Fox Brown, Lil Kim na Missy Elliott

Anao wakubali zaidi kwenye gemu :

Minaj alidai kuwakubali Jay Z, Foxy Brown na alishawahi kusema "nampenda sana Foxy kama rapa bora wa kike pia siwezi kukosa kumtaja Jay Z kama msanii bora wa kiume, tulipokuwa shuleni na wenzangu tulikuwa tukijifunza kuimba mistari ya Jay Z"

Kitu gani ambacho hawezi kusahau katika maisha yake? :

Minaj alidai kuwa hawezi kusahau kifo cha binamu yake Nicholas Telemaque ambaye alipigwa risasi karibu na nyumbani kwake huko Brookly, New York

Ananafasi gani ya utajiri :

Kwa mujibu wa Forbes ambayo hutoa tathimini juu ya uwezo wa wasanii ulimtangaza Minaj yupo katika matajiri kumi wa Hip Hop

Mwaka 2011 kwa mujibu wa Forbes Minaj alishika namba 8 kwa kuwa na utajiri unaofikia dola 15 milioni, kwa sasa utajili wake unaweza kuongezeka kutokana na mikataba kadhaa aliyoingia hivi karibuni

Maisha ya ugomvi :

Minaj alishawahi kuingia katika ugomvi na rapa Lil Kim baada ya rapa huyo kumtuhumu mwenzake kumuibia mistari yake kutoka katika kibao cha Pink Friday

Mbali na hayo hivi karibuni pia Minaj aliibuka katika ugomvi mwingine na muimbaji mkongwe Mariah Care

Gari la kwanza kumiliki :

Gari la kwanza kumiliki Minaj lilitokana na kuzawadiwa akiwa na umri wa miaka 19 baada ya kuchaguliwa kuwa muhudumu bora katika hoteli aliyokuwa akifanyia kazi

Kitu gani alikifanya cha ajabu? :

Alicheza picha ya ngono na kukiri hadharani huku akiwashauri wasichana kwa kuwaambia kuwa katika maisha ngono haiwezi kuepukika hasa kwa mabinti

Minaj ni wa aina gani ? 
Ni binti mwenye msimamo na kuna wakati alishatoa nyimbo mbili ambazo zinawatukana wanaume moja kwa moja

Anaabudu dini gani?
Minaj ni muumini mzuri wa dini ya kikistro, alishawahi kusema kuwa roho yake ipo kwa yesu ambapo mara nyingi hutumia mistari katika biblia



NICK MINAJ :PROFILE

Jina Kamili : Nika Tanya Maraj Jina analotumia kimuzik i : Nick Minaj Mahali alipozaliwa :  Alizaliwa Saint James Trinidad na ali... [Read More]




Jina lako halisi ?

C9: Jina nililopewa na wazazi wangu ni Charles Francis, ila jina la kazi naitwa C9 na ndilo lililozoeleka

Wewe ni mtoto wa ngapi kuzaliwa?

C9 : Mimi ni mtoto wa mwisho kati ya watoto watatu

Kabila gani ?

C9 : Mimi ni mngoni kwetu Songea

Elimu yako 

C9 : Nimeishia kidato cha sita baada hapo nikaingia chuo kilichopo Zanzibar kwa ajili ya kusomea maswala ya muziki

Kazi ya Producer uliianza lini?

C9 : Kazi hii niliianza mwaka 2004, huku nikiwa nimesoma maswala ya muziki Zanzibar, ambapo nilikuwa na ndoto lukuki za kukuza muziki wa kizazi kipya nchini

kitu gani kilikusababisha ukaingia katika upande wa utengenezaji wa muziki?

C9 : kwa sababu napenda sana muziki na nilikuwa napenda kuimba hiyo ndiyo sababu kubwa iliyonifanya niingie kwenye muziki ingawa hapo awali nilikuwa naimba

Sababu ipi ilikufanya uachane na uimbaji?

C9 : Mwalimu wangu ndiye aliyenishawishi nihamie upande wa utengenezaji wa muziki kwa sababu alikuwa ameona uwezo wangu ulikuwa ni mkubwa mno kwenye utengenezaji wa muziki kuliko kuimba

Changamoto gani unakumbana nazo katika kazi zako?

C9 : Da changamoto kubwa ambayo nakutana nayo ni pale msanii mkubwa yaani mwenye jina anapokuja studio kurekodi ngoma yake bila malipo yoyote wakati msanii chipukizi anakuwa na uwezo wa kulipia ngoma kwa bei kubwa ila yeye mkubwa anakuwa anazingua hiyo inasumbua sana tena muda mwingine inahalibu hadi uhusiano

Nyimbo ambazo zimekutambulisha kwenye gemu ni zipi?

C9 : One love ya Steven, Mama Ntilie hizi ni baadhi ya nyimbo ambazo zilinifanya nijulikane pamoja na kazi zangu kutambulika kijamii

Nyimbo gani ilikuwa ugumu sana studio?

C9 : Nyimbo iliyonipa ugumu ni Bao la Kete nyimbo ya AT kwa sababu kiwango alichokuwa anataka kufika ilikuwa bado sana na yeye alikuwa bado hajatambua nini afanya hilo ndilo lilikuwa ni tatizo kubwa

Ilikuchukua muda gani kuikamilisha nyimbo hiyo

C9 : ilinichukua muda wa wiki tatu kuikamilisha nyimbo hiyo kitu ambacho si cha kawaida sana kwa utengenezaji wa nyimbo

Msanii gani ambaye unatamani kufanya naye kazi?

C9 : Natamani sana kufanya kazi na msanii Lady Jaydee  kwa sababu anajua nini anafanya na anathamini kazi pamoja na nidhamu ya kazi anayo

Unajisikiaje unapotengeneza nyimbo alafu DJ wa redio anasema nyimbo haina kiwango ?

C9 : Huwa nawashangaa madj wa bongo kwani yeye hajui muziki ila anajidai anajua mimi ndiye ninayetengeneza muziki najua nataka utoke kwa kiwango gani yeye anavyoukataa namshangaa na wao ndio wanaoudidimiza muziki wetu

PROFILE : PRODUCER C9

Jina lako halisi ? C9: Jina nililopewa na wazazi wangu ni Charles Francis, ila jina la kazi naitwa C9 na ndilo lililozoeleka Wewe n... [Read More]




Ni ukweli usiopingika ukanda wa nchi za Afrika Magharibi ndiyo ukanda  pekee barani Afrika ambao umepiga hatua kubwa katika filamu za maigizo.

Ukweli huo unadhihirika wazi ukiangalia kazi  za wasanii wanaotoka ukanda huo hususani Ghana na Nigeria  mafanikio waliyonayo ni makubwa mno ukilinganisha na wasanii wengine barani humu.

Miongoni mwa wasanii hao ni Van Vicker,ambaye kwa kiasi kikubwa amepiga hatua kubwa kimaendeleo kupitia tasnia hiyo.

Kabla ya kuyaanika mafanikio yake kwanza tuangalie alipotoka  hadi kufikia hatua aliyopo kwa sasa.Historia inatuonesha kuwa  kwanza jina lake kamili anaitwa Joseph Van Vicker na ni raia wa Ghana ambaye alizaliwa Agosti mosi 1977 na baba yake mzazi ni Mholanzi na mama yake ni raia wa Liberia.

Kwa bahati mbaya baba yake alifariki  mapema sana wakati msanii huyo akiwa na umri wa miaka sita na kutokana na pigo hilo akalazimika kulelewa na mama yake tu na ndiyo maana hadi leo hii anamuhusudu mama yake akimuita shujaa  wake.

Kwa upande wa shule tunaelezwa kuwa Vicker, alisomea katika shule ya  Mfantsipim,ambako alisomea Katibu Mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa Koffi Annan, akiwa na msanii mwenzake  Majid Michel.

Baada ya kuhitimu masomo yake  mwaka 2003 ndipo alipoamua kujitosa katika sekta ya burudani kama mtangazaji wa redio na Televisheni Metropolitan na mwaka huo huo akatokea kwenye kipindi kilichokuwa kikitengenezwa na kurushwa palepale Ghana  kilichokuwa kikiitwa "Suncity" amabacho kilikuwa kikielezea maisha ya Chuo Kikuu

Katika kipindi hicho  aliigiza kwa jina  la LeRoy King Jr, akiigiza kama mwanafunzi wa chuo cha sanaa aliyezaliwa nchini Marekani na kwenda chuoni hapo Suncity kumalizia masomo yake.

Baada ya kufanya vizuri katika kipindi hicho ambacho kilikuwa na vipindi kumi  Van Vicker akapata mwaliko kama msanii msaidizi katika filamu yake ya kwanza iliyoitwa "Divine Love" ambamo humo alikutana na wakongwe waliokuwa wakifanya vizuri wakati huo kama Jackie Aygemang na Majid Michael.

Tunaambiwa kuwa filamu hii ndiyo ilimfungulia njia msanii huyo na tangu kipindi hicho akaanza kupaa na kupata mafanikio makubwa aliyonayo.

Vicker anadaiwa kuwa ni mkali wa filamu za mahaba na kwamba ndizo zinampatia soko kubwa ndani ya soko la Nigeria ikilinganishwa na kwao Ghana.

Kwa upande wa familia tunaambiwa kuwa Vicker ni baba mwenye nyumba kwani ameoa na ana watoto wawili

Kimafanikio Vicker yupo juu kwani anamiliki kampuni inaitwa Sky & Orange ambayo inashughulika na matangazo ya biashara ana pia kampuni nyingine inayoitwa  Babetown inayojihusisha na kuandaa matamasha mbalimbali pale Accra na ana bonge la salooni ya kiume aliyoipa jina la  Babetown.

Katika huduma za kijamii msani huyo pia hayupo nyuma kwani ana mfuko unaoitwa Van Vicker Foundation ambao unajihusisha na kuinua vipaji vya vijana katika sanaa.

Mwaka 2008 akipewa tuzo  muigizaji bora ya  African Movie Academy Award, ikiwa ni baada ya mwaka huo huo kukabidhiwa tuzo msanii bora anayechipukia.

Pia wa tuzo mwaka 2009 aliweza kuibuka msanii bora Afrika kwa upande wa filamu na hivyo kukabidhiwa tuzo ya Afro-Hollywood Award

VAN VICKER PROFILE

Ni ukweli usiopingika ukanda wa nchi za Afrika Magharibi ndiyo ukanda  pekee barani Afrika ambao umepiga hatua kubwa katika filamu za m... [Read More]



Wasifu wa P-Square ; Peter & Paul Okoye

Wasifu wa P- Square unaonesha kuwa Peter na Paul Okoye ni mapacha wametambuliwa zaidi kutokana na kazi zao za muziki kwa albamu zao kadhaa huku wakiwa chini ya leo ya Square.

Wamebaki pia kuwa wasanii bora wa muziki wa taratibu (R&B) Nigeria mwaka 2011, walihamia lebo ya Konviet muziki inayomilikiwa na msanii wa muziki wa Senegar aliyezaliwa Marekani anayetambulika kwa jina la Akon

Mwaka 2012 Psquare waliingia mkataba na msambazaji wa kazi chini ya lebo ya Afrika Kusini inayoitwa Universal Music, taarifa zinaonesha kwamba Psquare ni mapacha waliofanana wamezaliwa tarehe 18 mwezi wa kumi na moja mwaka 1981 kwa mantiki hiyo wanamiaka 30


Historia ya P-Square (PETER & PAUL OKOYE)

Kutokana na historia ya Psquare, wazazi wa Peter na Paul Okoye wanatokea jiji la Jos jimbo la Plateam kaskazini mwa Nigeria wakati Paul na Peter walisoma St Lumba elimu yao ya sekondari na walijiunga shule ya muziki na maigizo ambapo mapenzi yao ya kucheza na kuimba yaliendelezwa

Kikundi chao cha kwanza kilijulikana kwa jina la 'Smooth Criminals' na walitumbuiza maeneo tofauti jiji la Jos wakiwa na elimu ya juu

Tofauti ya Peter na Paul ni kwamba  Peter anapenda zaidi kuimba  huku Paul akipenda zaidi kucheza


Psquare na nyimbo za hivi karibuni na historia ya kisanii

Mziki wa hivi karibuni wa Psquare na unaonekana ukitamba zaidini Beautiful Onyinye ambao wameshirikisha msanii maarufu kutoka nchini Marekani Rick Ross video ya muziki imefanyika Los Angles na sasa wanashika kumi bora kwenye chati tofauti kama Nigeria, Uingereza pamoja na hayo walishinda tuzo za 'Grab the Mic' ambazo zilidhaminiwa na kuandaliwa na Berison na Hedges' mwaka huo huo kikundi 'Last Nite' album yao ya kwanza Psquare ilikuwa yamafanikio mwaka 2005 walitoa albamu ya pili ijulikanayo 'Get Squared' chini ya lebo yao 'Square Records'

Psquare

Video za muziki wa Psquare imekuwa ikichukua tuzo mbalimbali kutokana na ubora wa video hizo na aina ya uchezaji , mwaka 2007 walipata mafanikio ya uuzaji wa albamu kwa kuuza makala milioni 8,duniani

Albamu ya 'Game Over' mwaka 2009 walitoa albamu iliyokuwa inaitwa 'Danger' P-square wamechukua tuzo tofauti  kama BCT mwaka 2011MTV base mwaka 2010


Mashabiki wa Psquare wamekuwa wakijiuliza maswali juu ya mahusiani

Toka vyanzo vya habari hivi karibuni vinasema kuwa Peter hajafunga ndoa na Paul  Okoye pia mchumba wake ni mjamzito




P-SQUARE PROFILE

Wasifu wa P-Square ; Peter & Paul Okoye Wasifu wa P- Square unaonesha kuwa Peter na Paul Okoye ni mapacha wametambuliwa zaidi kuto... [Read More]





Jina lako kamili :

Linex : Naitwa Sunday Mseda Alias

Jina lako la utoto?

Linex : Nilivyokuwa mtoto walikuwa wananiita Sunday bishoo kwa sababu nilikuwa napenda sana kucheza mpira kwa mapozi sana na kwa fujo hadi marafiki zangu walikuwa wananichukia kwa sababu ya kutumia rafu sana kwenye mpira wa miguu

Safari yako ya muziki tangu utotoni ikoje?

Linex : Nimezaliwa katika familia ya muziki mama zangu wote wanaimba kwenye upande wa nyimbo za injiri hivyo hata familia yangu haikushangaa mimi kuwa muimbaji, na nilikuwa nipo nao bega kwa bega katika kazi hizo ya muziki nilijikuta naanza kuimba taratibu mpaka sasa

Safari yako ya muziki kwa kipindi hiki kabla haujajulikana ilikuwaje?

Linex : Nilikuwa napenda sana kutembelea bendi na nilikuwa nafanya mazoezi kwenye bendi mbalimbali za muziki na zilinipa changamoto sana mpaka hapa nilipo sasa

Muziki ulianza lini?

Linex : Nilianza muziki rasmi mwaka 2005

Nyimbo gani ilikutambulisha katika gemu ya muziki?

Linex : Nyimbo iliyonitambulisha katika gemu ya muziki ni Mama  Halima kwani mashabiki pamoja na wadau wa muziki walihisi mimi siyo mtanzania kwa mtindo niliyokuwa nimeutumia katika nyimbo hiyo

Umeshatoa jumla ya albamu ngapi?

Linex : Mpaka sasa nimetoa albamu moja ingawa nina albamu zaidi ya tano, siwezi kutoa nyingine kwani albamu hazilipi nitakuwa ninatoa single tu kwa ajili ya kutambulisha muziki na biashara kiujulma

Kwa nini unapenda kuimba nyimbo za hisia?

Linex : Napenda kuimba nyimbo za hisia kwa sababu nyimbo zangu zinatoka ndani ya moyo wangu, siwezi kuimba uongo, hivyo ninachokiimba ni kile kinachotendwa na watu wengi kwenye jamii, mfano mtu unayempenda utazungumza naye kwa hisia kubwa

Nini matarajio yako ya baadae?

Linex: Ni kuwa msanii mkubwa wa Afrika kwa sababu uwezo na nia ninayo na kuhakikisha malengo yangu ninayafanyia kazi ni pamoja na kujitahidi kutafuta nafasi ya kufanya kazi na wasanii wakubwa wa Afrika

Msanii gani wa Bongo anayekuvutia?

Linex : Wasanii wote wa bongo ninawapenda na wananivutia kikubwa ni kwamba yule anayefanya kazi yake vizuri kwangu mimi ni msanii bora

Kazi gani ya msanii unaipenda kuisikiliza kila mara?

Linex : Napenda kuisikiliza kazi ya msanii kutoka South Africa Zahara kwa sababu anaimba kama mimi kazi zetu zinafanana hicho ndio kikubwa kinachonivutia kusikiliza nyimbo zake

Kazi gani ya muziki kwako ilikuwa ngumu?

Linex : Ngwekewa ilikuwa kazi ngumu sana kwangu na ilinichukua muda mrefu sana kuikamilisha hususani kwenye upande wa video ilinichukua siku nne kuikamilisha kazi hiyo kwangu

Unauzungumziaje kila mtu kujiingiza katika tasnia ya muziki?

Linex : Uzuri wa sanaa haudanganyi na kizuri kinajionesha na bahati nzuri sasa watanzania wanajua kipi bora hivyo kila anayejiingiza katika tasnia hiyo azipokee changamoto hizo huku ahakikishe kuzifanyia kazi

Ni muda gani unaotumia kutunga nyimbo zako?

Linex : Mimi siafanyi muziki wa kutamba leo kesho ukapoteza ladha hivyo muda wangu mwingi huwa nafikilia muziki gani unaendana na misha halisi ya binadamu, kama nilivyokwambia muziki wangu unatoka moyoni hivyo ndivyo ninavyofanya kupata nyimbo bora, napata nafasi ya kujirekodi mwenye nyimbo kwanza kabla ya kuingia studio

Njia gani unatumia kupata jina la wimbo

Linex : Sijawahi kupata jina la wimbo wkati natunga nyimbo,nyimbo yangu ikishahisha ndipo jina linakuja

Unatumia kilevi chochote?

Linex : Situmii kilevi chochote kile na wala madawa ya kulevya situmii

Mahusiano gani yaliyokutesa sana?

Linex : Mahusiano yaliyonitesa sana nikwamba nilikuwa na mahusiano lakini umbali ndio lilikuwa ni tatizo kwetu na tuliachana kwa sababu hiyo, kwa upande wangu iliniwia vigumu sana kwa kuachana na mtu niliyekuwa nampenda kwa sababu ya umbali

Kazi gani unafanya tofauti na Muziki?

Linex : Mimi ni mfanyabiashara mdogo ninajihusisha na maswala ya biashara




LINEX PROFILE

Jina lako kamili : Linex : Naitwa Sunday Mseda Alias Jina lako la utoto? Linex : Nilivyokuwa mtoto walikuwa wananiita Sunday ... [Read More]



Jina lako halisi ni nani?

Recho: Jina nililopewa na wazazi wangu ni Rachael Haule, na la kisanii ni 'Recho' natumia hili zaidi ili kujitambulisha mimi mwenyewe na kazi zangu


Umezaliwa mkoa gani & mwaka gani?

Recho : Nimezaliwa mkoa wa Kigoma mwaka sitopenda kuuweka wazi


Kiwango chako cha elimu

 Recho : Nilisoma mkoani Kigoma ila niliweza kuishia kidato cha tatu, sikuweza kumaliza shule kwa sababu mbalimbali ambazo zilikuwa nje ya uwezo wangu, ila ninamshukuru mungu ninaweza kumudu maisha yangu ka elimu ndogo niliyoipata


Mtoto wa ngapi katika familia yenu?

 Recho : Mimi ni mtoto wa pili katika familia ya watoto wa wili wa  mzee Haule , kwa kifupi mimi ni( kitinda mimba) nikimaanisha ni mtoto wa mwisho


Je wewe ni kabila gani ?

Recho : Mimi ni Mmanyema

Utamaduni wa  kabila yako ni nini?

Recho: Ki ukweli sifahamu utamaduni wa kabila yangu, labda ni kwa sababu sijakaa sana mkoani

Unataka kitu gani kukifanya kwa kipindi hiki cha miezi mitatu?

Recho : Ni kutoa video ya wimbo wangu mpya wa 'Nashukuru' naamini utafanya vizuri katika gemu hili la muziki

Ni kitu gani unachokipenda kukifanya wakati huna kazi???

Recho : Napenda kushinda studio mara nyingi kama sina kazi ya kufanya, huku nasikiliza muziki na kutengeneza mawazo mapya wa muziki wangu na kunifanya nizidi kukuwa katika tasnia hiyo ya muziki

Unapenda mtindo gani ya nywele?

Recho : Napenda mtindo wa 'crazy' huwa unanifanya nionekane vizuri na kuzidisha urembo wangu zaidi

Je umeshawahi kushirikishwa kwenye kazi yoyote?

Recho : Nimewahi kushirikishwa na nyimbo ilitoka ila  haikufanya vizuri

Nini unachokiangalia zaidi katika sekta ya muziki wa Tanzania?

Recho : Naangalia muziki unaelekea wapi na mimi kuufwata muziki na si muziki kunifuata, namaanisha kuwa msanii unatakiwa ubadilike kulingana na mazingira na soko la muziki linataka nini,

Ni kitu gani unakikumbuza zaidi na kwa nini ?

Recho : Nakumbuka zaidi nilivyoanza kazi ya muziki yaani wazazi wangu walikuwa hawataki mimi niwe msanii na nilikuwa siwaelewi kabisa kwani nilikuwa ninapenda kuimba na kuwa msanii

Nini baadhi ya malengo yako ya baadae?

Recho : Kuwa mwanamuziki na siyo kuwa tena Recho, niwe ninauwezo mkubwa wa kufanya kazi nzuri zilizojaa ubunifu ndani yake

Mbali ya muziki unafanya kitu gani cha kuongeza kipato ?

Recho : Bado sijaanza kujihusisha na kitu chochote kile kwa sasa ninaukazania muziki wangu ili niweze kutimiza malengo yangu

Umeshatoa Albamu na kama bado unampango gani ?

Recho : Bado sijatoa albamu ila ninaandaa albamu yangu ya kwanza kwa sasa nina 'single' tatu, Upepo, Kizunguzungu na Nashukuru hizo ndizo nyimbo zangu ambazo zinasikika katika vituo vya radio mbalimbali

Unafikiria ni sehemu gani ya mwili wako ni bora na inakufanya uwe na mvuto ?

Recho : Sura yangu kiujumla ikiwa inazidishwa na macho yangu makubwa mazuri yanazidi kunionyesha ninamvuto na ni bora katika mwili wangu, pamoja na shepu yangu nzuri iliyoumbika vizuri inayosababisha nionekane vizuri ninapovaa nguo zangu

Jinsi gani unaweza kuelezea ulivyo kwa jamii?

Recho : Mimi ni mtu wa kawaida, mpole ninayependa kuzungumza na watu wa rika tofauti tofauti ninayependa kucheka, sina tabia ya kununa ovyo na huwa siipendi

Je ni kitu gani kuhusu wewe jamii ikisikia watashangazwa kujua ?

Recho : Napenda kudega ghafra tabia hiyo ninayo sana hata nikiwa nimekaa na marafiki zangu wakawaida tu huwa najikuta tabia hiyo ya kudeka ghafra inatokea

Unapenda mahusiano ya namna gani ?

Recho : Napenda ,mahusiano ya kipekee na si ya kuigiza, unamuona mtu yuko na mahusiano ya namna fulani na wewe unataka kuwa kama wao, hayo mimi siyapendi napenda mahusiano ya kipeke

Mwaka gani uliumizwa na mahusiano?

Recho : Ni mwaka huu tena hivi karibuni mwezi wa 8 niliumizwa sana na mahusiano na sipendi kuyaongelea




PROFILE: RECHO

Jina lako halisi ni nani? Recho: Jina nililopewa na wazazi wangu ni Rachael Haule, na la kisanii ni 'Recho' natumia hili za... [Read More]







Kama utataja majina kumi ya wasanii wa kike katika tasnia ya filamu nchini Nigeria, hutakosa kuligusa jina la mwanadada Omotola Jalade

Hii ni kutokana na uwezo mkubwa alionao katika tasnia hiyo na kuwa miongoni mwa waigizaji wa kike waliogiza filamu nyingi na kupata mafanikio makubwa

Mbali na tasnia ya filamu mwanadada huyo utamtaja pia katika fani ya muziki kutokana na umahiri wake katika sekta hiyo

Historia inatuonyesha kuwa Omotola Ekeinde Jalade ni mtoto wa familia ya watoto watano ya Bwana na Bibi Shola Jalade, ambao kwa sasa wote ni marehemu na ana kaka wawili Tayo na Bolaji Jalade

Omotola ambaye kwa sasa anasoma ya Utawala katika chuo cha Teknolojia cha Yaba, kilichopo mjini Lagos alifunga ndoa na Kapteni Matthew Ekeinde katika ofisi za msajili wa ndoa yao ndani ya ndege kutoka mjini Lagosi hadi nchini Benini April 19, 2001 ambapo hadi sasa wanandoa hao wana watoto wanne

Inaelezwa kuwa Omotola alianza kung'ara katika kijiji cha Nollywood baada ya kufyatua filamu aliyoipa jina la 'Mortal Inheritance' aliyoicheza mwaka 1995 ambako aliigiza kama mgonjwa mwenye matatizo ya ugonjwa wa Sickle-Cell ambaye anapigania uhai wake licha kuwa anafahamu hatapona ,ingwa siku alipona na kupata mtoto na hatimaye aliendelea kuishi

Filamu hiyo amabyo ilikubalika iliweza kupata tuzo na tunaelezwa kuwa hadi sasa bado inafahamika kuwa ni miongoni mwa filamu bora nchini Nigeria

Tunaelezwa kuwa tangu kipindi hicho mwanadada huyo hakuweza kugeuka nyuma ambapo aliendelea kufyatua filamu kali kali kama vile 'Games Women Play' 'Blood Sisters', 'All my life' na nyinginezo kabala ya mwaka 2005 kujitumbukiza kwenye kazi ya muziki

Katika fani ya muziki mwaka 2006 alifyatua albamu yake aliyoipa jina la 'Gba'

Zifuatazo ni filamu ambazo msanii huyo ameweza kuzifyatua

Ties That Bind (2011)
A private Stom
Ije: The Journey (2010)
My Last Ambition(2009)
Beyonce&Rihanna(2008)
Temple of Justice(2008)
Tomorrow Must Wait(208)
Yankee Girls(2008)
Careless Soul(2007)
Desperate Sister(2007)
Final War(2007)
Sand in My Shoes(2007)
Sister's Heart(2007)
The Prince of My Heart(2007)
The Revelatio(2007)
Titanic Battle(2007)
Tota War(2007)
Brave Heart(2005) hizo ni baadhi ya filamu alizocheza msanii huyo

OMOTOLA JALADE ANAYETINGISHA TASNIA YA FILAMU NIGERIA

Kama utataja majina kumi ya wasanii wa kike katika tasnia ya filamu nchini Nigeria, hutakosa kuligusa jina la mwanadada Omotola Jala... [Read More]



Miaka ya 80 hadi 93, ni kipindi ambapo kilikuwa kinasisimua kiburudani , hali hiyo ilikuwa inatawala kizazi kipya cha muziki wa 'Soukous' kutoka nchini zaire(sasa DRC ) hasa baada ya kumalizika kwa enzi ya za akina Luambo Makiadi (Franco)

Ikumbukwe kipindi hiko miongoni mwa wanamuziki waliokuwa wakitamba ni kama Aurus Mabele, Lokasa ya Mbongo, 'Mzee Benz' Bozi Boziana, Scola Miel na mtindo wao wa Nzawisa

Utamu wa sauti kutoka kwa Lucian Bokilo na utundu wa kucharaza gitaa wa Dally Kimoko ulitosha kabisa kupagawisha watu mpaka wanasahau kama kuna kesho

Kwa wale ambao walikuwa wapenzi wa kwenda viwanja ikumbukwe kipindi hicho kiwanja kilichokuwa kikitamba ni Tazara Hostel ambapo wakati muda fulani watu wameshaanza kuchoka anapandishwa hewani 'Mzee wa Fujo' Alan Kounkou na baada ya sekunde kadhaa Jean Baron anaingia na kibao chake cha 'Mami Lolo'

Hata hivyo huwezi kuwazungumzia wanamuziki hao bila ya  kuligusia gwiji la kucharanga gitaa, Diblo Dibala, ambapo kwa kawaida anafahamika kama Diblo au kwa jina lingine 'Machine Gun' kutokana na kasi yake ya kucharaza gitaa

Historia inaonesha kuwa Diblo alizaliwa mwaka 1954 mjini Kisangani na baadae akahamia katika mji wa Kinshasa wakati huo alikuwa mtoto

Tunaelelzwa kuwa akiwa na umri wa miaka 15, alishinda mashindano ya kusaka vipaji ambapo kutokana na umahiri wake wa kucharaza gitaa ulimfanya ajiunge na bendi ya marehemu Franco, TPOK Jazz

Hata hivyo alikaa na kundi hilo kwa muda mfupi na baadae akaenda kushilikiana na makundi ya Vox Afrika, Orchestra Bella mambo na Bella Bella ambapo bendi yake ya kwanza ilikuwa ya Kanda Bongo Man

Mwaka 1979 alihamia mjini Brussels, Ubelgiji kabla ya mwaka 1981 kujiunga na bendi ya Kanda Bongo Man mjini Paris Ufaransa amabapo alifyatua albamu yake ya kwanza mwaka huo na kuipa jina la Lyole

Tangu kipindi hicho Diblo alizidi kupanda chati hususani baada ya kufanya kazi na wanamuziki kama Pepe Kale na makundi mengine mengi yaliyokuwa yakipiga muziki wa Soukous

Mwaka 1980 aliamua kuunda bendi yake aliyoipa jina la Loketo ambapo alikuwa akishirikiana na mwanamuziki Aurlus Mabele , hata hivyo miaka michache baadaye bendi hiyo ilivunjika hali ambayo ilimlazimu mwaka 1990 kuunda kundi jipya alilolipa jina la Matchatcha, ambalo hadi sasa linaendelea kufanya kazi baada ya kulifanyia marekebisho mbalimbali

DIBLO DIBALA GWIJI LA KUCHARAZA GITAA

Miaka ya 80 hadi 93, ni kipindi ambapo kilikuwa kinasisimua kiburudani , hali hiyo ilikuwa inatawala kizazi kipya cha muziki wa 'Sou... [Read More]


 Leo tunatua nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasiya ya Kongo DRC ambapo tunakutana na mwanamama Elisabeth Tshala Miana ,mwanamama huyo ni miongoni mwa wanamuziki wa kike barani Afrika wenye historia ndefu katika tasinia ya muziki wa kiafrika

Kwa mujibu wa historia yake Muimbaji huyo raia wa DRC zamani Zaire alizaliwa mjini Lubumbashi mnamo mwaka 1957,Tshala alianza kazi yake ya muziki mnamo mwaka 1976 mjini Kinshasa akiwa mnenguaji wa bendi mpya kwa kipindi hiko ya M’pongo Love ambapo baada ya miaka miwili akiitumia bendi hiyo aliamua kujiunga ya Minzoto Wella ambapo nako alikaa miezi michache akiwa mmoja wa wanafunzi wa Abeti Maskini

Akiendelea na kibarua chake cha kuimba hakuachana nacho hadi alipoondoka Congo Kinshasa ambayo na kwenda kutafuta maisha Ivory Coast. Mwaka 1981 akiwa mjini Abidjan mwanamama huyo alianza kuimba akiwa na bendi moja iliyokuwa ikiongozwa na raia wanchi hiyo

Hata hivyo kama ilivyoada kwa wasanii wengi husani wanamuziki umaarufu wa mwanadada huyo ulipatikana pale alipotua mjini Paris akiwa na mwanamuziki Hyacinthe, wakiwa na nyimbo zao kama ‘Amina’ wimbo ambao ulikuwa na miondoko ya Pop na ambao uliimbwa kwa lugha ya kifaraza ukisaidiwa na mwingine wa ‘Tshebele’ ambao ulikuwa kwenye maadhi ya mutuashi ambalo asili yake ni kabila La Baluba waishio kusini mwa DRC ndizo zilizompaisha mwanamuziki huyo

Inaelezwa kuwa albamu na matamasha mbalimbali ambayo bendi hiyo iliyafanya ndani na nje ya Ivory Coast ndiyo yalimfanya yazidi kumpaisha katika tasinia hiyo , mwaka 1984 Tshala alihamia mjini Paris ambako teyari eneo hilo lilishakuwa kituo cha kutayarisha nyimbo kwa wanamuziki wa kizaire

Akiwa mjini Paris alifanikiwa kurekodi albamu yake ya kwanza aliyoipa jina la ‘Kami’ akiwa na raia wa Cameroon Aladji Toure na Kisha baadaye akarekodi albamu nyingine mbili Mbanda Matiere (Tatizo la wapinzani) na nyingine aliyoipa jila la M’Pokolo kwa lugha ya kifaransa, Le petiti Ruisseau likiwa ni maana kwa lugha ya Kiswahili mkondo mdogo

Albamu hiyo ya M’Pokolo iliandaliwa na mwanamuziki Toure wakimshirikisha mpiga gitaa mashuhuri raia wa Kongo DRC ,Rigo Star,hata hivyo mara nyingini Tshala alikuwa akijiiandikia kazi yake tofauti na ilivyo kwa wanamuziki wa kizaire kupendelea kuimba kwa lugha ya kilingala na kucheza mtindo wake wa rumba na ule wa Soukous , Tshala aliibuka na mtindo wake wa mutuashi ambapo kwa mara ya kwanza aliimba kwa kutumia lugha ya Tshiluba

Akiwa ameshajijenga jina ndani ya Abidjan na Paris, mwaka 1986 Tshala alirejea mjini Kinshasa na kujiandalia matamasha yake binafsi , hata hivyo licha ya kupata mapokesi makubwa baada ya kuwasili nchini humo tatizo la uchumi kuwa mgumu lilimfanya ashindwe kuendelea na kibarua chake nchini humo na hivyo kumlazimu Tshala kubaki makao yake makuu yakiwa mjini Paris ambapo walau kila mwaka aekuwa akifyatua albamu moja huku akifanya ziara Ulaya na Afrika



TSHALA MWANA PROFILE

 Leo tunatua nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasiya ya Kongo DRC ambapo tunakutana na mwanamama Elisabeth Tshala Miana ,mwanamama huyo ni ... [Read More]

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging