Msanii ambaye ni mremavu wa ngozi (Albino), amekuwa kivutio katika shoo ya Epiq Bongo Star Search 2012(EBSS), iliyoonyeshwa jana katika kituo cha ITV, KIjana huyo alikuwa na mvuto wa aina yake kwa kuwa mbali na kuwa na hali hiyo ya ulemavu wa ngozi lakini alijitambua na kuamini kuwa anaweza
Msanii huyo chipukizi anaimba na vijana wenzake ulemavu wa ngozi na pia mara nyingi hualikwa katika tamasha la sauti za busara , anaonekana kuwa na shauku ya kuja kuwa msanii wa kimataifa siku za baadaye ambapo majaji wa mashindano hayo wameamua kumvhagua katika hatu ya 50 bora
Licha ya msanii huyo pia kulikuwa na msichana mdogo anayesoma shule ya Sekondari Makongo aliimba wimbo wa Mwasiti wa THT msaniii huyo wa kike katika mahojiano yake alisema malengo yake ni kuwa msanii wa kimataifa na alianza kujifunza muziki miaka mine iliyopita
Washiriki waliofanikiwa kuingia katika 50 bora ya EBSS 2012 kwa mkoa wa Dar es Salaam ni wale ambao inaonekana wanaufahamu vyema muziki