Google PlusRSS FeedEmail

DOTNATA BAADA YA KUUMWA SASA AOKOKA


Msanii maarufu kwenye tasinia ya filamu Husna Posh ‘Dotnata’ ambaye pia ni mjasiriamali amefunguka na kusema kuwa aliugua kwa muda mrefu lakini maombi yalimsaidia kupona ,Akizungumza juzi usiku alisema kuwa muda mrefu alikuwa anasumbuliwa na matatizo ya miguu kuuma, lakini anamshukuru mungu maombi yaliyokuwa yakifanyika yalimsaidia kupona

“Leo natoa ushuhuda kuwa maombi niliyokuwa naombewa katika madhehebu ya Kikiristo yamenisaidia kuweza kurudi kwenye hali yangu ya ya kawaida” alisema

Alisema ametumia tiba mbalimbali pamoja na dawa za wachina lakini bado hazikuweza kufua dafu hadi alipoamua kuingia kwenye maombi ambayo yalimponyesha na kurejea katika hali yake ya kawaida

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging