Msanii mkongwe kwenye tasnia ya filamu nchini Nuru Nassoro ‘Nora’ amefunguka kwa kusema kuwa anawaomba wadau wa filamu nchini kuwatumia wasanii wenye vipaji na nia ya uigizaji
Nyota huyo alisema kuwa wadau wa tasnia hiyo wamekuwa wakiwasahau wasanii chipukizi ambao wapo katika vikundi na kuwachukua wageni ambao baadae wanakosa muelekeo
“Nashangaa mastaa tuliopo kwenye ‘gemu’ la tasnia hii vipaji vyetu vilianza chini mpaka kufikia hapa tulipo, kumetokea suala la wasanii wanaoandaaa filamu zao kushirikisha mtu kutoka nyumbani na kumpatia nafasi ya ushiriki kwa ghafla na kuacha kupita kuangalia vipaji vya chipukizi waliojiandaa kwenye vikundi hali hii inaweza kuharibu tasnia “ alisema
Aliongezea kuwa yeye mpaka kufikia kung’ara alitokea kwenye maonesho ya fashion shoo na Taji Liundi ndio alimshauri kuingia rasmi kwenye fani ya uigizaji