FILAMU YA MWISHO YA KANUMBA KUINGIA SOKONI
Filamu ya mwisho ya marehemu Steven Kanumba ambayo mwenyewe alibatiza jina la ‘Ndoa yangu’ itaingia sokoni septemba 28 mwaka huu na kusambazwa na kampuni ya usambazaji ya Steps Entertainment
“Filamu ya Ndoa Yangu inatarajia kutoka hivi karibuni baada ya kutengenezwa katika ubora wa hali ya juu pia tunatumia filamu hiyo kutambulisha ufungaji mpya wa filamu zinazotoka kampuni ya Steps Entertainment tutakuwa na package mpya kabisa ambayo si rahisi kwa maharamia kutumia , wito ni wadau wetu kutambua alama mpya za filamu halali” inasema taarifa ya Steps Entertainment
Filamu ya Ndoa Yangu ni kazi inayotegemea kuteka soko la filamu baada ya muda mrefu bila ya kutoa filamu zilizoigizwa na marehemu kanumba ,katikafilamu hiyo pia utakutanana na mwanadada Jack Wolper
Ndoa yangu ni filamu ya mwisho aliyocheza marehemu Kanumba siku chache kabla ya kufariki ,kwa walioiona wanasema ni kama alikuwa akijitabiria kifo chake kwani mengi aliyoyaigiza yanafanana na mazingira ya kifo chake