GOLDIE AMFUATA PREZZO KENYA
Aliyekuwa mmoja wa washiriki na wawakilishi wa Nigeria katika jumba la Big Brother Stargame 2012 Goldie jumamosi iliyopita aliwasili katika nchi ya Kenya mida ya usiku . Goldie alipokelewa uwanja wa ndege na Prezzo kitu kinachowafanya watu wengi waamini kuwa sasa uhusiano kati ya Prezzo na Goldie umerejea katika hali nzuri,sambamba na Prezzo pia alikuwepo pia mshiriki mwingine wa Big BrotherMillicent Mugadi
Muda mfupi baada ya Goldie kuwasili uwanja wa ndege mabegi yake yalipelekwa katika Mercedz Benz E-Class rangi ya silver ya Prezzo ambayo ndiyo iliyompeleka katika hotel aliyofikia, ujio wa Goldie nchini Kenya umekuwa wa kimya kimya kitu kinachoashiria kuwa yeye pamoja na mwenyeji wake hawakupenda nukuu ya vyombo vya habari
Kwa mujibu wa watu wa karibu wa Prezzo Goldie amesema atakuwa Kenya kwa muda wa wiki nzima au na zaidi na lengo la safari yake hiyo kufanya recodi ya nyimbo na kati ya nyimbo atakazo recodi anategemea kumshirikisha Prezzo