Sony Music Entertainment Afrika imetangaza kusaini mkataba na mshindi wa jumla wa tuzo za muziki nchini Uganda rapa Keko,mpango huo ni wa kwanza kufanyika kati ya mwanamuziki kutoka nchini Uganda kusaini matengenezo ya albamu na usimamizi kamili wa mpango huo na kampuni hiyo kubwa ya kurekodi
Keko ataungana kwenye orodha ya wasanii wa kimataifa katika studio hiyo ya ya Sony RCA, ambayo inafanya kazi na mastaa wengine wakiwemo kina Alicia Keys, Pink, Usher, Christina Aguilera, na Chris Brown
Rapa huyo mwenye kipaji ambaye anaongoza kwa Afrika Mashariki anavibao kadhaa vyenye mashiko,kupanda kwa umaarufu wake ulianza mwaka 2010 baada ya kutoa kibao cha Fallen Heroes ambapo alionekana akiwa sambamba na wasanii wengine kutoka Uganda kama Don MC, SP, Davis na The Mwamba Children Choir