Mchakato wa kusaka washiriki wa Shindano la Maisha Plus na Mama Shujaa wa Chakula 2012 mkoani Mwanza unatarajia kufanyika leo katika Hoteli ya Stone Club
Shindano hilo ambalo limedhaminiwa na Benki ya NMB ,Oxfam pamoja na marafiki zake msimu huu limeboreshwa zaidi ambapo watanzania watashuhudia akipatikana Mama Shujaa wa Chakula 2012 na baadaye mshindi wa Maisha Plus
Tayari mchakato wa kuwasaka washiriki wa Shindano hilo umeshakamilika kwa upande wa pwani, Tanga, Kilimanjaro, Arusha , Manyara na Dodoma na sasa zoezi hilo limeamia mkoani Mwanza
Akizungumza jana mkuu wa kitengo cha Ubunifu wa Maisha Plus Francis Bonda ‘Kaka Bonda’ aliwataka vijana wote wa kazi mkoani hapo wenye umri kati ya miaka 21-26 ambao wanapenda kushiriki shindano hilo wajitokeze kwa wingi katika hoteli ya Stone Club kuanzia saa tatu asubuhi
Bonda alisema baada ya hapo wataelekea mkoani Kagera wilwya ya Kargwe ambako mchakato wa kuwasaka washiriki wa shindano hilo utafanyika septemba 5 mwaka huu
“Baada ya kutoka Karagwe tutaelekea moja kwa moja Kahama mkoani Shinyanga ambapo zoezi hilo litaendelea kabla ya kurudi Dar es Salaam
“Ikumbukwe kwamba kinachofanyika sasa hivi kwa upande wa washiriki wa mashindano haya ni usaili hivyo baadaye tutapitia huku vigezo na masharti vikizingztiwa kabla ya kutaja washindi ambao watakwenda moja kwa moja kijijini “ alisema Bonda
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Maisha Plus Masoud Kipanya aliwataja washiriki wa Mama Shujaa wa Chakula 2012 ambao wamefanyiwa usaili ni watano kati ya kumi na tano wanaotakiwa kushiriki