MASANJA ARUHUSU KUNAKILIWA KAZI YAKE
Mwimbaji wa muziki wa Injili nchini Emmanuel Mgaya 'Masanja Mkandamizaji' amesema kuwa albamu yake iitwayo 'Hakuna Jipya' ametoa kibali watu kunakili bure,ili ujumbe ufike kwa urahisi zaidi kwa watu
Akizungumza Dar es Salaam alisema hali hiyo ya kuwaruhusu wadau kunaliki bure itasaidia kufikisha ujumbe wa kiroho kwa watu wote
"Watu wanatakiwa kuokoka wakiwa na nguvu na si wasubili wakati kifo au kuugua, kwa mtu yoyote awe msanii ama mfanyabiashara inampasa kuokoka akiwa na nguvu zake"alisema
Aliongezea kuwa amekuwa akipokea ujumbe kutoka sehemu mbalimbali kuhusu kazi yake na ameomba watu wengine wajitoe katika kazi ya kumtukuza mungu