Tamasha hilo ambalo litafanyika kwa siku mbili Ijumaa na Jumamosi, litafanyika katika viwanja vya Leaders Klabu, Dar es Salaam na kushirikisha bendi 12.
Akizungumza Dar es Salaam jana mratibu wa tamasha hilo, Edwin Ngere alisema kwamba watakaobahatika kupata tiketi hizo watachagua sehemu yoyote wanayotaka kwenda.
"Hii yote ni katika kuwapa raha na burudani mashabiki wa muziki wa dansi watakaofika katika tamasha hili," alisema mratibu huyo. Alisema katika kuhakikisha tamasha hilo linakuwa la aina yake bendi zote zitakazoshiriki zimejichimbia mafichoni kujifua zaidi wakiwa na lengo kutoa burudani ya nguvu.
Mratibu huyo alisema pia katika tamasha hilo kiingilio kitakuwa sh. 5,000. Alisema siku moja kabla ya tamasha hilo kutafanyika majaribio ya jukwaa jipya la kisasa, ambalo litazinduliwa rasmi.