CPWAA KUVALISHA NA SHERIA NGOWI
Msanii anayetamba kwenye tasnia ya muziki wa Bongo Fleva Tanzania Cpwaa ameingia katika mkataba wa kuvalishwa na mwanamitindo , Sheria Ngowi, katika video zake zote
Msanii huyo ambaye ni tishio katika tasnia hiyo alisema ameingia mkataba wa kutangaza mavazi ya mwanamitindo huyo
Cpwa alisema mbali na kumtangazia mavazi yake, pia atakuwa akivaa nguo hizo pindi anapotengeneza video zake mpya kuanzia sasa
Aliongezea kuwa alianza kuvaa nguo za mwanamitindo huyo mwaka jana ambapo hivi karibuni aliamua kuingia naye mkataba wa moja kwa moja