Google PlusRSS FeedEmail

MDOGO WA KANUMBA SETH BOSCO AFANYA KWELI KWENYE FILAMU YA MALAIKA

Seth Bosco ambaye ni mdogo wake na msanii nyota aliyetikisa tasnia ya filamu nchini marehemu Steven Kanumba amekusudi kufunika pengo liloachwa na marehemu kaka yake  msanii huyo amesema katika kumuenzi kaka yake atahakikisha kuwa kampuni inaendelea na kufanya kazi za filamu zenye ubora wa hali ya juu...“Baada ya kumaliza msiba na taratibu zingine kampuni ya Kanumba Great Film inaendelea na kazi zake kama awali na kufanya katika ufanisi wa hali ya juu, nakumbuka wosia wake juu yangu na kwa kufuata hayo namuenzi kwa kutengeneza filamu ya Malaika ambayo mimi ni mhusika,”Seth licha ya kuwa ni mdogo wake na marehemu lakini pia ndio aliyekuwa mtu wa karibu na marehemu Kanumba, katika filamu hiyo ya Malaika Seth anaigiza na mwanadada Rose Ndauka ambaye pia aliwahi kufanya kazi na marehemu, wasanii wengine wanaoshiriki katika filamu hiyo ni Abdalah Mkumbila ‘Muhogo Mchungu’, Maya na wengine wengi.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging