MUIGIZAJI TOM CRUISE APONDA RAHA UINGEREZA
Muigizaji Tom Cruise ameendelea kujirusha katika jiji la Londen nchini Uingereza akiwa peke yake, Tom hivi karibuni ameingia katika matatizo na familia yake baada ya kutengana na mke wake jambo linalosababisha hata asiwe karibu na mke wake
Tom hana maisha ya raha na sasa ameamua kuhamia nchini Uingereza ambapo huko amekuwa akiendelea kujirusha katika kumbi mbalimbali
Mwisho mwa wiki hii Tom Cruise alionekana akitoka katika Hoteli ya Ivy akiwa peke yake huku mashabiki kadhaa wakionekana kutaka kuzungumza naye jambo ambalo liliwapa wakati mgumu walinzi wake